Katibu wa mbunge wa jimbo la Ludewa Bw.Fungatwende akifungua mafunzo hayo katika ukumbi wa ccm wilaya ya Ludewa.
Viongozi wa vikundi mbalimbali vya sanaa kutoka vijiji vya wilaya ya Ludewa wakifuatilia mafunzo hayo
Viongozi wa vikundi mbalimbali vya sanaa kutoka vijiji vya wilaya ya Ludewa wakifuatilia mafunzo hayo
Viongozi wa vikundi mbalimbali vya sanaa kutoka vijiji vya wilaya ya Ludewa wakifuatilia mafunzo hayo
Steven Mapunda akitoa somo katika mafunzo hayo kwa viongozi wa wasanii wilayani Ludewa.
Wasanii
wilayani Ludewa wametakiwa kuwa na umoja ili kukuza sanaa yao ambayo
itaitangaza wilaya ya Ludewa na Taifa kwa ujumla kwani wilaya ya Ludea
inahazina kubwa ya vipaji zikiwemo ngoma za asili ambazo hazipatikani maeneo
mengine nchini.
Hayo
yamesemwa na Mbunge wa wilaya ya Ludewa Mh.Deo Ngalawa kupitia katibu wake
Bw.Fotunartus Fungatwende hivi karibuni katika mafunzo ya siku moja yaliyofanyika
katika ukumbi wa chama cha mapinduzi Ludewa yaliyoandaliwa na Ludewa Talent
Program na kuratibiwa na Ludewa Youth Talents.
Akifungua
mafunzo hayo Bw.Fungatwende kwa niaba ya Mbunge ambaye alialikwa kuwa mgeni
rasmi katika mafunzo hayo ya kujengewa uwezo alisema kuwa wilaya ya Ludewa
inahazina kubwa ya vipaji vya wasanii lakini vipaji hivyo vinashindwa kuonekana
kutokana na kutokuwa na umoja wa wasanii.
Alisema watu
wa maeneo mengine wamekuwa wanahamu ya kuona tamaduni za wanaludewa lakini
hawapati fulasa hiyo kutokana na baadhi ya wasanii waliofanikiwa kuwa wabinafsi
kwa kushindwa kuwainua wengine ili waweze kuitangaza wilaya yao.
“vijana kwa
wazee kunafulsa kubwa ya kujikwamua kiuchumi kupitia sanaa zenu lakini kuna
baadhi ya watu wakishafanikiwa husahau nyumbani,mimi nimshukuru Steven Mapunda
kupitia Ludewa Talent Program na kwa kushirikiana na kikundi cha sanaa cha
Ludewa Youth Talents kwa kufanya mafunzo haya ambayo yameweza kuwakutanisha
wasanii wa sanaa mbalimbali kutoka vijiji vya Ludewa na kwa kufanya hivi umoja
unaweza kupatikana”,alisema Bw.Fungatwende.
Bw.Fungatwende
alisema kuwa Steven Mapunda ni msanii mkubwa wa Bongo Muvi lakini richa ya kuwa
tayari ameshafanikiwa aliona si vyema akabaki na ujuzi huo Jijini Dar akaona
arudi nyumbani na kuongea na wasanii wengine ili nao siku moja wafanikiwe kama
yeye.
Alisema kuwa
kwa kuonesha umoja huo na nia ya kutengeneza Filamu ya pamoja na ngoma za asili
ambayo itaendelea kitambulisha wilaya ya Ludewa Mh. Ngalawa atawaunga mkono kwa
asilimia mia ili kuhakikisha umoja huo unaendelea kudumu na kuinua sanaa zote
za nyumbani zinawanufaisha wasanii.
Aidha msanii
Steve Mapunda mwenyekiti wa Ludewa Talent Program ambaye alitokea jijini Dar es
Salaam ambaye ni mzaliwa wa wilaya ya Ludewa akitoa mafunzo hayo ya kuwajengea
uwezo wasanii wa wilaya ya Ludewa alisema kuwa aliona sio busara kukaana ujuzi
huo mjini bali jambo la msingi ni kugawana na wasanii wa nyumbani bila kujali
kila mmoja anafanya sanaa ipi.
Bw.Mapunda
alisema kuwa inauma sana kuona kunawasanii wakubwa wa kutoka wilaya ya Ludewa
wamefanikiwa lakini hawarudi nyumbani kuwainua na wenzao kwani mfano mzuri ni
wasanii wa Kigoma wamekuwa wakisaidiana na kufanya kazi ya pamoja na kuutangaza
mkoa wao.
Alisema kuwa
tayari mpango wa kurekodi ngoma za asili na kuziuza umekamilika pia mpango wa
kurekodi Filamu yenye mahadhi ya wilaya ya Ludewa unaendelea kukamilika kwani
unatarajia kugharimu kiasi cha shilingi milioni saba na nusu hivyo mchakato wa
kuomba wadau mbalimbali ili kufanikisha kazi hiyo unaendelea.
Naye Mwenyekiti
wa Ludewa Youth Talents Bw.Nasibu Luoga aliwataka wasanii wa wilaya ya Ludewa
kupitia vikundi vyao au msanii mmoja mmoja kujisajiri katika baraza la sanaa la
Taifa kama kikundi chake kilivyosajiriwa kwani kwa kufanya hivyo uwezo wa
kupata mikopo ya vikundi ili kuendeleza sanaa itawezekana.
Bw.Luoga
alisema kuwa kikundi cha Ludewa Youth Talents baada ya kusajiriwa kimenufaika
na mambo mengi yakiwemo mafunzo mbalimbali yanayotolewa katika kazi ya
wilaya,Mkoa hadi Taifa hivyo vikundi vya ngoma za asili na sanaa kwa ujumla
vinatakiwa kusajiriwa ili viweze kutambuliwa na Serikali.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment