Hawa ndio baadhi ya wanafunzi wa Ludewa Education Center wakiwa na mratibu wao Bw.Mwinuka
Mratibu wa Ludewa Education Center Bw.Augustino Mwinuka akiwa n badhi ya wanafunzi wake
Hawa ndio baadhi ya wanafunzi wa Ludewa Education Center wakiwa na mratibu wao
Mratibu wa Ludewa Education Center Bw.Augustino Mwinuka akiwa n badhi ya wanafunzi wake
Kituo kipya
cha Ludewa education center kilichopo Ludewa mjini katika ukumbi wa ccm
kimekuwa mkombozi wa elimu wilayani hapa kutokana na kituo hicho kupokea watu
wa rika zote ili kupata elimu kwa muda mfupi kwa gharama nafuu.
Akiongea na
mtandao huu leo mratibu wa kituo hicho Bw. Augustino Mwinuka alisema kuwa licha
ya kuwa jamii ya Ludewa imeona kituo hicho ni suruhisho la watu wasio na vyeti
vya kidato cha nne lakini kimekuwa kikipokea wanafunzi wa kidato cha kwanza
kutoka vijiji vyote vya Ludewa.
Bw.Mwinuka
alisema kuwa wilaya ya Ludewa kwa mika mingi imekuwa haina jituo hivyo kama
wilaya nyingine nchini na kwa kuona hilo yeye na wenzie waliamua kuanzisha
kituo hicho ili kuweza kutoa elimu kwa wale wanaotaka kujiendeleza kielimu na
kwa wanaotafuta vyeti vya kidato cha nne na kupata sifa ya kuendelea na kidato
cha tano hadi sita na baadae chuo kikuu.
Alisema
kituo hicho kilianza mwaka 2016 na awali jamii haikuwa na mwamko wa kujiunga
katika kituo hicho lakini hivi sasa baada ya kuona mafanikio ya baadhi ya
wanafunzi wanaosoma hapo watu wamekuwa wengi mpaka uhitaji wa kuongeza madarasa
umeanza kuonekana.
“tulianza
kama utani lakini kwa sasa wazazi wanawaleta watoto wao kupata elimu hapa pia
wafanyakazi mbalimbali wamekuwa wakisoma katika kituo cheti ili kutafuta sifa
za kuendelea na kidato cha tano na baadae chuo kikuu,hivyo tunapenda kuwaeleza
wazazi na jamii kwa ujumla nafasi bado tunazo na elimu tunayoitoa inakubalika
pia QT na wanaorudia mitihani ya kidato cha nne wanapokelewa”,alisema
Bw.Mwinuka.
Bw.Mwinuka
aliwataka wadau wa eliu kuiga mfano huo ili kuhamasisha jamii ya Ludewa na
Tanzania kwa ujumla hasa vijijini ambako kielimu kumekuwa nyuma tofauti na
maeneo ya mijini.
Kwa mawasilino
wasiliana na mratibu wa kituo kwa namba 0765059184
Mwisho.
No comments:
Post a Comment