Jeshi
la Polisi limeongeza muda wa huruma kwa wamiliki wa silaha walioshindwa
kuhakiki silaha zao katika zoezi la uhakiki wa silaha za kiraia
Tanzania Bara lililoanza Machi 22 na kumalizika Juni 30, 2016.
Kaimu
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai CP Robert Boaz, amesema
licha ya Jeshi la Polisi kuongeza muda wa uhakiki hadi mwezi Oktoba
mwaka huu, bado wamiliki wengi hawakujitokeza kuhakiki silaha zao.
“Katika
kipindi cha kuanzia tarehe 22 Machi, 2016 hadi Juni 30 serikali ilianza
kufanya zoezi la uhakiki wa silaha zote za kiraia hapa Tanzania Bara,
kutokana na sababu mbalimbali tuliongeza muda lakini bado baadhi ya watu
hawakujitokeza,” amesema.
Amesema
baada ya zoezi la awali kukamilika, tathmini inaonyesha kuwa asilimia
59.18 ya silaha zote zilizosajiliwa ndizo zilizohakikiwa na kwamba
asilimia 40.82 hazijahakikiwa.
CP
Boaz amesema polisi imeongeza muda wa mwezi mmoja ili wasio hakiki
silaha zao wahakiki, na kwamba muda huo ni wa mwisho hautaongezwa tena.
“Tunatoa
tena muda wa huruma tunawataka wamiliki wajitoekeze vituoni kuhakiki
silaha zao ndani ya mwezi mmoja kuanzia Novemba 21 hadi Disemba 20,
2016. Huu ni muda wa mwisho na utakapomalizika tutachukua hatua kali.”
Amezitaja
baadhi ya hatua zitakazochukuliwa ikiwa ni pamoja na kufuta leseni za
umiliki kwa silaha zote zisizohakikiwa, kuwatangaza wamiliki wote wa
silaha kwenye vyombo vya habari walioshindwa kuhakiki pamoja na
kuwafikisha katika vyombo vya sheria.
Ametoa
wito kwa wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha silaha zao
katika vituo vya polisi au ofisi za serikali za mitaa na kwamba atakae
tumia kipindi hiki hawatachukuliwa hatua za kisheria.
No comments:
Post a Comment