Katibu wa Ludewa Tinsmith Bw.Bahati Mtweve
Hivi ni baadhi ya vifaa vinavyotengenezwa na kikundi hicho
Shirika
lisilo la kiserikali lenye makao yake makuu wilayani Ludewa katika mkoa wa
Njombe lijulikanalo kwa jina la Ludewa Tinsmith linalojihusisha na utoaji elimu
mbalimbali kwa vijana ikiwemo elimu ya ufundi limewataka vijana kujikita zaidi
katika kujiajiri kuliko kutegemea ajira kutoka Serikalini ili kujiingizia
kipato.
Akitoa
taarifa hiyo ofisini kwakwe Mwenyekiti wa shirika hilo Bw.Vianely Ngailo
alisema kuwa idadi kubwa ya vijana waliosoma
vyuo vikuu na vyuo vya kati wamekuwa wakishindwa kuendesha maisha yao
kwa kusubiri kuajiriwa na Serikali wakati zana hiyo sio sahihi kwani wanapaswa
kubuni miradi itakayopelekea kujiajiri na kuwaajiri wengine ili kujipatia kipato
Bw.Ngailo
alisema kuwa Ludewa Tinsmith inajishughurisha na mambo mbalimbali ikiwemo
utoaji wa elimu ya ufundi kwa fani za,useremala,ushonaji,umakenika na uungaji
vyuma ambapo richa ya elimu hiyo ya ufundi pia inatoa elimu ya ujasiliamali kwa
watu wanaoishi mazingira magumu ili waweze kujitegemea au kutembea kwa miguu
yao wenyewe kiuchumi.
Alisema kuwa
shirika hilo lilianzishwa mwaka 1988 lakini limepata usajiri rasmi mwaka 2013
na mpaka sasa limeshafundisha vijana zaidi ya 98 ambao wanawake wanakadiriwa
kuwa 38 na wanaume 60 wenye mazingira
magumu ambao mpaka sasa wanaendesha maisha yao bila kuwa tegemezi kwa watu
wengine au Serikali.
“tungependa
vijana wenzetu nchini waige mfano wetu wa kujiajiri wenyewe wanapohitimu elimu
ya vyuo kuliko kutegemea serikali kuwaajiri,sisi tunaamini tukijiajiri tunaweza
kuzarisha ajira kwa wengine kwakuwafundisha ufundi na kuwaajiri wengine ambao
tunaweza kufanya nao kazi kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeisaidia Serikali
kwa kiasi Fulani”,alisema Bw.Ngailo.
Bw.Ngailo alisema
kuwa shirika hilo linalojiendesha kwa michango ya wanachama richa ya kuwa
nitafanya kazi zake bila ya kuwa na ufadhiri wowote nimekuwa likiandika
maandiko kuomba vitendea kazi kwa wafadhiri bila mafanikio lakini limekuwa
likikabiriwa na changamoto kubwa ya eneo la kufanyia kazi hizo za ufundi kwa
limekuwa likipanga katika majengo ya watu hali inayo walazimu wakati mwingine
kuingia matatani kutokana na wenye majengo kuwafukuza wakidai huchakaza nyumba
zao.
Bw.Ngailo
aliiomba Serikali ya wilaya ya Ludewa kutoa Ardhi kwa wadau wa maendeleo kama
wao ili waweze kujenga viwanda vidogo vidogo vitakavyowasaidia vijana kujenga
ofisi zao ikiwemo na madarasa ya kufundishia kwa vitendo katika viwanda hivyo
vidogo.
Aidha mkuu
wa wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya alikiri kuchelewa kwa mpango wa utoaji
wamaeneo ya viwanda vidogovidogo wilayani hapa hali inayowafanya vijana wengi
kushindwa kujiendeleza katika kazi zao za kujitafutia kipato lakini mpango huo
upon a utakamilika hivi karibuni ili vijana hao wafanye kazi zao kwa uhuru.
Bw.Choya
aliwataka vijana wilayani Ludewa kuiga mfano wa shirika la Ludewa Tinsmith
katika kuzalisha ajira kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wameongeza ajira kwa
vijana wenzao ambao siku zote wamekuwa wakiwa na dhana ya kusubiri kuajiriwa na
Serikali.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment