Saturday, March 19, 2016
Chadema Yawafuata CCM Mahakamani....Yapinga Agizo la Jiji La Dar Kuwazuia Wananchi Kuingia Kwenye Ukumbi wa Uchaguzi wa Meya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema hakikubaliani na
agizo la serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Jiji la kuwataka wanaotakiwa
kuhudhuria kwenye kikao cha uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam
wawe ni wajumbe pekee watakaopiga kura.
Chama hicho kimekataa agizo hilo na badala yake kinataka wananchi wote wa jiji la Dar es salaam wahudhurie katika kikao hicho.
Msimamo huo wa Chadema unapingana na barua ya wito wa mkutano wa
uchaguzi huo iliyoandikwa Machi 15, 2016 na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la
Dar es Salaam, Sarah Yohana, iliyosema kuwa watakaoruhusiwa kuingia
katika viwanja hivyo ni wajumbe pekee ambao ni wapigakura.
Akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa
wa Dar es Salaam, Mwita Waitara alisema sheria na kanuni zinaruhusu
wananchi kushiriki kikao hicho cha wazi, hivyo Yohana hana mamlaka ya
kuwazuia.
“Sisi tunafuata sheria na kanuni, barua ya mkurugenzi inaeleza kinyume cha utaratibu,” alisema.
Alisema kufuatia hali hiyo, Ukawa umemwandikia barua Mkurugenzi
huyo ya kutokubaliana na matakwa yake ya kuzuia wafuasi wa vyama kuingia
ukumbini wakati wa uchaguzi kwani ni uvunjifu wa sheria na kwamba
hawatakubali, bali watawapigania na kuhakikisha wananchi wanaingia
ukumbini.
Katika hatua nyingine, Waitara alisema CCM kwa sasa inawaandaa wanachama feki wa CCM
wakiongozwa na wakili Elias Nawela kufungua kesi ya madai huku wakitaka
wajumbe 9 toka Zanzibar na 11 kutoka mikoa mingine kushiriki uchaguzi wa
meya.
Alisema,
ili kukabiliana nao, wameamua kuwafuata hukuhuko mahakamani ambapo
tayari wameshatuma maombi ya kujiunga na kesi hiyo namba 39 ya mwaka
2016 huku wakiwa na mawakili wao ambapo inatarajiwa kusomwa Machi 21
mwaka huu katika Mahakama ya Kisutu.
No comments:
Post a Comment