Dkt.Suzan Kolimba akiongea na wanawake wa Ludewa
Dkt.Suzan akikumbatiana na diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monika Mchilo
kiongozi wa soko la samaki Ludewa mjini AKIMSHUKURU Dkt.Suzan
Anayecheka ni mbunge mstaafu na mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ludewa Bw.Stanley Kolimba,katikati ni mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Anatory Choya na aliyevaa shati ya kijani ni katibu wa ccm wilaya ya Ludewa Bw.Lusiano Mbosa
Naibu waziri wa wizara ya mambo ya
nje ya nchi na ushirikiano wa Afrika mashariki mabaye pia ni mbunge wa viti
maalum katika mkoa wa Njombe Dkt.Suzan Kolimba amewataka wananchi wa wilaya ya
Ludewa na mkoa wa Njombe kwa ujumla kwenda na kasi ya utendaji kazi wa Rais wa
Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ili kujinasua na umasikini
ulio kithiri.
Dkt.Suzan aliyasema hayo hivi
karibuni wakati wakitimiza ahadi yake ya ukarabati wa soko la samaki wilayani
Ludewa ambapo alitoa rangi lta miamoja na arobaini pamoja na saruji mifuko
ishirini ili kuweza kulikarabati soko hilo ambalo kwa muda mrefu lilisahaulika
hali ambayo ilileta sura mbaya ya mji wa Ludewa.
Aliwataka wananchi wote kwa umoja
wao kuchapa kazi za kilimo na ufufugaji kutokana na wilaya ya Ludewa kuwa na
ardhi nzuri kwaajili ya kilimo na ufugaji kwani kwa kufanya hivyo umaskini
uliokithiri wilayni hapa utaondoka mara moja hasa wanawake ambao ndio walezi wa
familia ndio ambao pia hufanya biashara ya samaki nyasa katika soko hilo la
samaki.
Dkt.Suzan alisema kuwa wananchi wa
wilaya ya Ludewa wanasifika katika utendaji kazi na ndio wilaya pekee katika
mkoa wa Njombe inayozalisha zao la mahindi na maharage kwa wingi hivyo wakati
umefika sasa hata kwa wanasiasa kuwa na maneno kidogo kazi zaidi ili kuwakwamua
wananchi kiuchumi hasa wananchi walioko vijijini.
“Napenda kuwakumbusha wananchi wa
wilaya ya Ludewa hasa akina mama wenzangu kuwa tufanye kazi na tutumie
kaulimbiu ya maneno kidogo kazi zaidi ili kujiletea maendeleo kwani licha ya
mimi kukamilisha ahadi yangu ya ukarabati wa soko hili la samaki ambalo akina
mama ndio wafanyabiashara wakuu pia nawahimiza tujikite katika kilimo ambacho
ni mkombozi wa maisha ya walio wengi”,Alisema Dkt.Suzan.
Alisema kutokana na utendaji mzuri
wa Rais Dkt.Magufuli ni dhahili maendeleo yenye tija yatawafikia wananchi wote
hadi wale waliokatishwa tamaa na ugumu wa maisha kule vijijini hivyo wananchi
wanapaswa kuliombea Taifa na kumuombea Rais pia kumuunga mkono katika mambo
mazuri anayoyafanya kwa kufanya kazi kwa bidii ili kuondokana na umaskini.
Akishukuru kwa utekelezaji wa ahadi
hiyo ya Naibu waziri Diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monika Mchilo alisema kuwa ni
jambo lisilo pingika kuwa utendaji wa viongozi wakuu wanchi unatia moyo hali
inayowafanya wananchi nao kujikita zaidi katika uzalishaji kwani kila mmoja
anaona na sio kusikia tu utendaji huo.
Mh.Monika alisema kuwa ukarabati wa
soko hilo utailetea heshima wilaya ya Ludewa pamoja na wafanyabiashara ambao
idadi kubwa ni akina mama wanaofanya biashara ndani ya soko hilo hivyo hawana
la ziada zaidi ya kuwaunga mkono viongozi wakuu wanchi kufanya kazi kwa bidii
katika kila sekta.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment