Bw.Lusiano Mbosa akimshukuru Mh.Ngalawa kwa msaada wake wa shilingi milion tano
Mh.Deo Ngalawa akifanyiwa maombezi maalum
Mh.Deo Ngalawa akifanyiwa maombezi maalum
hizi ndizo nyumba za wachungaji ambazo Mh.Ngalawa alichangia fedha ya ukarabati kiasi cha shilingi milioni mbili
Mh.Deo Ngalawa akiongea na waumini wa kanisa la Lutherani Ludewa mjini
Mh.Deo Ngalawa akiongea na waumini wa kanisa la Lutherani Ludewa mjini
Mbunge wa
jimbo la Ludewa katika mkoa wa Njombe Mh.Deo Ngalawa ametoa mchango wa shilingi
milioni tano katika Kanisa la Kiluteli Ludewa Mjini,fedha hizo milioni mbili ni
ukarabati wa nyumba mbili za wachungaji na milioni tatu ni mchango wa gari
ambayo inatakiwa kusaidia huduma za kichungaji katika Kanisa hilo wilayani
Ludewa.
Akitoa fedha
hizo katika maombezi maalumu yaliyofanywa na Kanisa hilo ili kumuombea mbunge
huyo kufanya kazi kwa ufanisi Mh.Ngalawa alisema kuwa wilaya ya Ludewa
inahitaji watu wanaoweza kubuni miradi ambayo itaweza kuwakwamua waumini wa
dini mbalimbali kiuchumi hivyo ni vema wachungaji wakaanza kutoa elimu hiyo kwa
waumini wao.
Mh.Ngalawa
alisema kuwa Kanisa hilo limeonesha kuwa linamipango mizuri ya kujitegemea
kutokana na hali halisi ambayo imeonesha katika mishango inayotolewa na kila
muumini siku ya ibada hivyo yuko tayari kuwaunga mkono wale wote wenye malengo
ya kuibua miradi katika vikundi mbalimbali.
Alisema kuwa
kasi ya kimaendeleo wilayani Ludewa bado iko nyuma kutokana na ugumu wa maisha
unaowakabili wananchi wa wilaya ya Ludewa hiyo ndiyo sababu ya mtangulizi wake
hayati Deo Filikunjombe enzi za uhai wake alikuwa mkali sana Bungeni na
alisimamia ukweli kwa maslahi ya wanaLudewa hivyo kila mwananchi wa jimbo hili
anapaswa kukaza buti katika kuharakisha maendeleo mingoni mwa jamii.
“Nimeupenda
mfumo wenu wa kuchangishana fedha kwa uchache wenu mumeweza kuzijenga nyumba
hizi za wachungaji hivyo nami nawaunga mkono kwa kutoa shilingi milioni mbili
katika ukarabati pia natoa milioni tatu ili kuharakisha ununuzi wa kari ya
mchungaji ambayo itamsaidia kutoa huduma maeneo mbalimbali ya wilaya yetu”,alisema
Mh.Ngalawa.
Mh.Ngalawa
aliwataka washirika wa makanisa na Dini nyingine wilayani hapa kuiga mfano huo
ambao unamalengo mazuri ambayo wisho wa siku itakuwa ni chachu ya kimaendeleo
kwa wilaya nzima kwani unafundisha namna ya kujitegemea na kuachana na
wafadhiri ambao hutoa fedha zao zikiambatana na masharti magumu.
Akishukuru
kwa msaada huo kwa niamba ya waumini wa Kanisa hilo ambaye pia ni mzee wa Kanisa
la Kirutheli wilayani Ludewa Bw.Lusiano Mbosa alisema kuwa Kanisa hilo
linampango wa kujenga nyumba ya wageni ili kujiingizia kipato hivyo huo ni
mwanzo tu wa safari yao ya kujitegemea.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment