Vijana sita wa JKT Bulombora, Kigoma Wafariki dunia Baada ya gari la Jeshi kushindwa Kupanda mlima na Kupasuka tairi
VIJANA sita waliokuwa katika mafunzo ya kijeshi ya kujitolea katika kikosi cha 821 JKT Bulombora mkoani Kigoma wamefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa vibaya kutokana na ajali ya gari iliyotokea jana jioni
Mganga Mfawidhi wa hospital ya mkoa wa Kigoma Dkt. Fadhil Kibaya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
"Ni
kweli jana majira ya saa moja jioni tumepokea miili minne ya vijana wa
JKT ambao waliletwa hapa tayari wamefariki na majeruhi 21.
"Wengine wawili wamefariki hapa hapa wakati tukiendelea kuwapa huduma" alisema Dkt Fadhili.
"Wengine wawili wamefariki hapa hapa wakati tukiendelea kuwapa huduma" alisema Dkt Fadhili.
Alisema hali za majeruhi mpaka sasa siyo nzuri sana kwani wengi wameumia sehemu za kichwa na mwilini.
"Bado tunaendelea na jitahada za kuwapatia matibabu na majina ya waliopoteza maisha pamoja majeruhi tutatoa kesho, sababu majeruhi wengi hawana fahamu"alisema.
"Bado tunaendelea na jitahada za kuwapatia matibabu na majina ya waliopoteza maisha pamoja majeruhi tutatoa kesho, sababu majeruhi wengi hawana fahamu"alisema.
Naye
kamanda wa polisi mkoa wa kigoma Afande Ferdinand Mtui alisema chanzo
cha ajali hiyo ni gari hilo la jeshi kushindwa kupanda mlima na
kusababisha tairi mbili za nyuma kupasuka.
Alisema
ajali hiyo ilitokea katika eneo la Kasaka karibu na mizani ambapo lori
hilo la jeshi lilikuwa likitoka mjini kwenda kambini likiwa limebeba
makreti ya soda na unga.
No comments:
Post a Comment