Leo
tarehe 29 October 2015, kwa kupitia Mgombea Mwenza wangu, Mh. Juma Duni
Haji nimewasilisha rasmi malalamiko yetu kuhusu mwenendo mzima wa
uchaguzi mkuu wa 2015 kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Tumeainisha
kwenye malalamiko yetu, kutokuridhishwa kwetu na mwenendo na matukio
mbalimbali, hususani, utangazaji wa matokeo batili, yasiyo akisi matokeo
halisi yaliyopatikana kwenye vituo vya kupiga kura, kama ifuatavyo.
• Upunguzwaji wa kura zangu
• Kuongeza kura kwa mgombea wa CCM
•Tunaendelea
kukataa dhuluma hii dhidi ya matakwa ya wananchi, na jaribio la kutaka
kubakwa kwa Demokrasia kunakooneka wazi kutokana na mwenendo wa Tume
kuendelea kutangaza matokeo ya kura yasiyo ya kweli kwa kupoka ushindi
wetu.
Aidha, kumekuwepo pia na uporaji wa ushindi kwa wagombea wa vyama vya UKAWA kwenye ngazi ya Ubunge na Udiwani
Kama
tulivyoeleza jana takwimu zetu sisi zilionesha kwamba nilikua naongoza
kwa zaidi ya 67%,na sasa tumejiridhisha kwamba nimepata kura 10,268,795 sawa na asilimia 62% baada ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu za matokeo nchi nzima.
Kwa hali hii, ninaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi initangaze mara moja mimi EDWARD NGOYAI LOWASSA kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Kwa hali hii, ninaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi initangaze mara moja mimi EDWARD NGOYAI LOWASSA kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Naendelea
kuwashukuru wananchi kwa imani yenu kwangu na kunichagua, MImi, pamoja
na viongozi wenzangu tunaamini kuwa kuchezea Demokrasia ni kuvunja
Amani, lakini sote tunatambua ni nyie watanzania ndio mnaoporwa haki
yenu ya kupata mabadiliko, na viongozi mnao wahitaji, hivyo nitaendelea
kuwa pamoja na watanzania wote kudai haki yenu kwa nguvu zote.
Tanzania
kwa miaka mingi imefahamika kama kisiwa cha amani katika Afrika,
tunashangaa leo kuona vyombo vya ulinzi na usalama vikitanda kila mahali
wakiwa na silaha za kivita mitaani kana kwamba uchagzui ni vita, hii ni
kuwatisha wananchi ili wakubali kunyang’anywa haki yao ya msingi ya
kuchagua viongozi wanao wataka, nina amini watanzania hatutakubali hali
hiyo.
Lowassa, Edward Ngoyai.
29.10.2015
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment