Hawa ndio watendaji wa vijiji 77,wenyeviti wa vijiji na watendaji wa kata za wilaya ya Ludewa walipokutana katika mkutano wa kuhamasisha maendeleo katika ukimbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa
Mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe akiongea na viongozi hao wa kata na vijiji
Mzee maarufu na mkongwe wa siasa ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa Mzee Hilali Nkwera akiongea na viongozi hao
WENYEVITI wa
vijiji vyote 77 vya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wametoa
tathimini yao ya utendaji wa mbunge wa jimbo la Ludewa
Deo Filikunjombe na kumhakikishia ushindi wa kishindo uchaguzi mkuu
utakaofanyika Octoba mwaka huu na kuomba chama cha mapinduzi (CCM)
kuwaeleza wanachama wake wanaotaka ubunge kuelezwa wazi
kuwa nafasi hiyo imejaa.
Wenyeviti hao
ambao baadhi yao ni wale waliotokana na vyama vya
upinzani walitoa kauli hiyo jana wakati wa semina
ya ujasiliamali iliyoandaliwa na mbunge huyo kwa wenyeviji wote 77 na
watendaji wote wa serikali za vijiji 77 na kufanyika katika ukumbi
wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa .
Akizungumza kwa niaba ya
wenyeviti hao Bw Andrew Mwafute alisema kuwa
jitihada zilizofanywa na mbunge Filikunjombe katika wilaya ya
Ludewa ni kubwa na kila mwananchi wa Ludewa na wasio wa
Ludewa ambao wanafika wilayani humo ni mashahidi wa maendeleo
ya sasa ya wilaya hiyo wanatambua mchango mkubwa wa
mbunge huyo katika maendeleo hivyo hawana sababu ya kutafuta mbunge
zaidi nje ya Filikunjombe kwa sasa na kama ingekubalika wao wasingehitaji
uchaguzi wa mbunge ..
" Sisi
wenyeviti wa vijiji ambao ni wawakilishi wa wananchi pamoja
na watendaji wa vijiji tunatamka wazi kuwa utendaji kazi
wetu umekua rahisi zaidi katika wilaya ya Ludewa
kutokana na kazi kubwa inayofanywa na mbunge wetu ..... mbunge
Filikunjombe katika kila kijiji mradi wowote wa maendeleo kuna
mchango wake wa asilimia kama si 70 basi 90 hivyo sisi
tunapata faraja zaidi katika kutekeleza miradi hiyo na wananchi
kutowachosha na michango "
Bw Mwafute alisema
kwa kazi iliyofanywa na mbunge huyo katika jimbo la
Ludewa kwa kipindi cha miaka 5 ni kubwa zaidi na
imezidi hata ile ya wabunge waliokaa madarakani zaidi ya miaka 40 bila
kufanya kazi kubwa kama hiyo ya mbunge wa Ludewa.
Hata
hivyo alisema ili Ludewa izidi kusonga mbele zaidi
hakuna sababu ya wana Ludewa kufanya siasa kama ilivyo
maeneo mengine siasa za kuvutana kwenye mambo ya maendeleo kwani
kufanya hivyo ni kujikwamisha zaidi katika maendeleo na
kuwa lazima CCM kuwa na zoezi la kuwatathimini wabunge ,madiwani
wao na kama wamefanya kazi chini ya kiwango wakimaliza
kipindi kimoja wasiruhusiwe kupewa fomu tena ila waliofanya vizuri
ndio waruhusiwe kuwa wagombea pekee ndani ya chama .
Mwenyekiti
wa serikali ya kijiji cha Luana Bw David Luoga
alisema kwa mfano katika kijiji chake kazi zilizofanywa na
mbunge huyo ni kubwa zaidi na kwa kawaida wananchi wake
ni wenye msimamo wa kutochagua mbunge ama diwani kwa
kipindi cha pili kama ameshindwa kutatua kero zao ila wao kwa
upande wa mbunge hawahitaji mwana CCM mwingine zaidi ya mbunge wao .
Alisema kamwe
hawatamsahau mbunge huyo kwani ameweza kuwaharakishia
maendeleo ya kijiji hicho kwa kufikisha umeme na
kuwatengenezea barabara hiyo ya Malatu - Itungi ambayo
ilikuwa haipitiki japo inaelekea katika taasisi mbali mbali kama
nyumba za ibada, soko, Zahanati na shule ila serikali ya
wilaya haikuona sababu ya kuitengeneza hadi wananchi
hao walivyoomba kwa mbunge huyo katika mkutano wao wa
hadhara uliofanyika miezi mitatu iliyopita .
Bw Luoga
alisema toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961
kijiji hicho hawajapata barabara nzuri kama hiyo iliyojengwa na
mbunge wao umbali wa kilomita 2 iliyogharimu kiasi cha zaidi ya Tsh
milioni 54 barabara muhimu ambayo haikupewa umuhimu wowote na
serikali ya wilaya ya Ludewa.
Hivyo alisea
ahsante yao kwa mbunge wao kwa kuwaletea maendeleo ni
kuona wanamchagua kwa kura nyingi zaidi ili kuendelea kuwa
mbunge kwa vipindi vingine 15 ama zaidi na kuwa kipimo
chake kilikuwa ni miaka mitano hii ambayo ameonyeha
ufaulu wa zaidi ya asilimia 100 hivyo kama kijiji wananchi
wameweza kuchangishana na kupata kiasi cha Tsh 100,000
kwa ajili ya kwenda kuchukulia fomu muda wa
kufanya hivyo utakapofika.
Pia waliomba
utaratibu ulioanzishwa na mbunge huyo wa kuwakutanisha
mwenyeviti na watendaji wote wa vijiji pamoja kama
hivyo uendelee na miaka mingine badala ya kuwaacha
wenyeviti peke yao huku madiwani wakiwa na baraza lao na kukutana
mara kwa mara wakati msimamizi mkuu wa maendeleo kijijini ni wao na sio
madiwani .
Kwa upande
wake mbunge Filkunjombe pamoja na kuwapongeza
wenyeviti hao kwa kumpa faraja zaidi bado alisema wenye
mamlaka ya yeye kuendelea kuwatumikia ama kutowatumikia ni
wananchi wenyewe na hadi sasa bado ubunge anautamani na lengo
kubwa kuzidi kuleta maendeleo zaidi ya hayo katika
wilaya ya Ludewa na kueleza moja kati ya sababu ya kujivunia
kuendelea kuwa mbunge ni ile ya kutekeleza ahadi zake zote
alizopata kutoa kwa wananchi wakati wa kampeni mwaka 2010.
Alisema
wananchi wa Ludewa bila kujali itikadi zao wamekuwa bega kwa bega
kushirikiana katika shughuli za kimaendeleo na kupongeza pia
wenyeviti wa vijiji na watendaji kwa kujitoa kwa nguvu zote
kusimamia miradi ya kimaendeleo .
Aidha mbunge
huyo alimuagiza mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Ludewa iwapo
ataendelea kuwa mbunge wa Ludewa kumuandalia kusanyiko la wenyeviti
hao na watendaji kila baada ya miaka miwili japo kwa mara moja ili
kubadilishana mawazo .
Mwisho.
No comments:
Post a Comment