Dkt.Nchimbi akizindua uthaminishaji na ulipwaji fidia
Mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt.Nchimbi akicheza ngoma na wananchi wa Kijiji cha Mundindi
Filikunjombe akiongea na wananchi
wananchi wakifuatilia mkutano
hiki ndicho chuma cha linganga
Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Ludewa ikimsikiliza mkuu wa mkoa wa Njombe
Mkuu wa mkoa wa Njombe Dkt Nchimbi,Mh.Filikunjombe,mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Choya,mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Bw.Fredrick Mwakalebela pamoja na mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba akiangalia makaa ya mawe Nchuchuma
viongozi mbalimbali wakiangalia makaa ya mawe
haya ndio makaa ya mawe Nchuchuma
kikundi cha ngoma ya mganda kikisubiri kutumbuiza
mkuu wa wilaya ya Ludewa Anatory Choya akiangalia mkaa wa mawe
Mkuu wa mkoa
wa Njombe Dkt.Rehema Nchimbi amezindua rasmi zoezi la uthaminishaji na ulipwaji
wa fidia kwa wananchi wanaotakiwa kuhama ili kupisha ujenzi wa miradi mikubwa
ya machimbo ya chuma cha pua Liganga na makaa ya mawe Nkomang’ombe iliyoko
wilayani Ludewa zoezi ambalo litafanyika
haraka kutokana na wawekezaji wa miradi hiyo kuwa tayari kwa kazi.
Akifanya
zoezi hilo la uzinduzi jana na leo katika maeneo ya Liganga na Nchuchuma Dkt
Nchimbi aliwataka wathaminishaji kutenda haki kwani wananchi wa maeneo hayo
wamefanya uungwana wa kuyatunza madini hayo kwa miaka mingi bila malipo yoyote
kutokana na shirika la maendeleo la taifa kuwazuia kufanya uendelezaji wa
maeneo yao tokea mwaka 1982.
Dkt.Nchimbi
alisema Serikali imezamilia kuanzisha miradi hiyo haraka baada ya kufanya
utafiti kwa muda mrefu na kujiridhisha katika utafiti huo hivyo tayari fedha za
kuwalipa fidia wananchi wenye mashamba na miti na baadhi yao wenye nyumba
watahamishwa kwa kulipwa fidia za mashamba na kujengewa nyumba za kisasa.
Alisema
katika jambo hili la ulipwaji fidia hakuna siasa kwani wananchi wamechoshwa na
ahadi hivyo amewaonya wanasiasa kukaa mbali na jambo hilo kwani yeyote atakaye
leta siasa katika jambo zito kama hilo sheria itachukua mkondo wake haraka
iwezekanavyo.
“wananchi wa
maeneo ya migodi hii mnakila sababu ya kupewa sifa na Mwenyezi Mungu awabariki
kwa kutunza raslimali hii kubwa ya Taifa letu kwani miradi hii itawanufaisha
watanzania wote ila nawaomba wanasiasa kutoingilia jambo hili waacheni
wathaminishaji wafanye kazi yao kwa uaminifu mkubwa na hatimaye wananchi hawa
walipwe fidia zao”,alisema Dkt.Nchimbi.
Akisoma
lisala ya wananchi wa kijiji cha Nkomang’ombe katika uzinduzi wa uthaminishaji
na ulipwaji fidia kwa wananchi Bw.Yusuf Mwazayo alisema kuwa wananchi
wanafuraha kubwa kusikia ujenzi wa miradi hiyo ambayo imekuwa ikitajwa kwa
miaka mingi bila mafanikio inaanza kwani ni fulsa pekee kwa wanaludewa kujitoa
katika wimbi la umaskini.
Bw.Mwazayo
alisema kuwa richa ya kuwa mananchi wamejawa na furaha ya uanzishwaji wa miradi
hiyo lakini shirika la maendeleo la Taifa (NDC)linapaswa kutafakari upwa kwani
kwa miaka mingi wananchi wamekuwa wakizuiwa kuendeleza maeneo yao kutokana na
maeneo hayo kuwekwa alama ili kulipa fidia baadaye lakini imekuwa ndivyo sivyo
kutokana na NDC kuchukua maeneo machache tu.
Alisema
kinachotakiwa ni kuvilipa vijiji fidia ili wananchi ambao hawatakuwa katika
eneo la mradi waweze kunufaika na malipo hayo kwani ni muda mrefu wameshindwa
kufanya maendeleo yao binafsi.
Aidha Mbunge
wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe amewataka wathaminishaji wa maeneo hayo
kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa kutokana na maeneo mengi wananchi kuilamu
Serikali kwa kuandamana kudai haki zao ambazo hundurumika na baadhi ya
wathaminishaji wasio waaminifu.
Mh.Filikunjombe
alisema kuwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais
Jakaya Mrisho Kikwete ni Serikali makni nayowajali wananchi wake hivyo
imewaamini wataalamu watakaofanya kazi ya uthaminishaji hivyo wataalamu
hawapaswi kuingiza maslahi yao na kuichafua Serikali iliyowaamini.
Aliwataka
NDC kuwakabidhi wananchi maeneo yao kupitia Serikali za vijiji kwani kwa muda
mrefu maeneo hayo yamekuwa yakimilikiwa na NDC na kuahidi watawalipa wananchi
fidia lakini imeonekana hayana kazi tena hivyo wananchi wanayahitaji maeneo yao
ili wapate kuyaendeleza katika shughuri za kimaendeleo
Mwisho.
No comments:
Post a Comment