Hiki ni kikosi cha mtaa wa Majengo
Hizi ni timu za mitaa ya Majengo na Kilimahewa na timu ya mtaa wa Kilimahewa iliibuka kidedea
Hawa ni vijana wa mtaa wa Mkondachi
Mtaa wa mkondachi wakiwa na viongozi wao
Vijana wa mkondachi wakifanya mazoezi ya viungo
Vijana wa mkondachi wakifanya mazoezi ya viungo
Vijana wa mkondachi wakifanya mazoezi ya viungo
Vijana wa mkondachi wakifanya mazoezi ya viungo
Vijana wa mkondachi wakifanya mazoezi ya viungo
Ligi mitaa
ya mpira wa miguu katika kata ya Ludewa imeendelea kutimua vumbi huku ikiwa na
ushindani mkali ambao haujawahi kutokea kwa kila mtaa umekuja na vipaji vipya
hali ambayo mpaka sasa kwa wataalamu wa kupanga matokeo wanashindwa kutabiri
nani anatibuka kidedea.
Ligi hiyo imeanzishwa
na diwani wa kata ya Ludewa Mh.Monica Mchilo ambapoa ameweza kugawa vifaa vya
michezo kwa kila mtaa vikiwa ni jezi na mpira mmoja na zawadi kwa washindi
ikiwa mshindi wa kwanza ataibuka na kiasi cha shilingi laki mbili wakati
mshindi wa pili anatapata shilingi laki moja na nusu na watatu laki moja.
Akifungua
mashindano hayo hivi karibuni Mh.Mchilo alisema lengo la mashindano hayo ni
kuibua vipaji kwani ameona afanye hivyo kutokana na timu nyingi za mji wa
Ludewa zimekuwa zikisaka vipaji kutoka wilaya na kata jirani pale zinapotakiwa
kushiriki mashindano makubwa katika ngazi ya mkoa na Taifa wakati kata hiyo
inavipaji vya kutosha.
Mh.Mchilo
aliwataka wachezaji kujenga undugu katika mashindano hayo na kuondoa tofauti
zao kwa siku zote michezo ni furaha na amani.
Katika
mzunguko wa kwanza wa mashindano hayo timu zilizofuzu ni ,mtaa wa Kilimahewa,Kiyombo,Kanisa
A na Kanisa B pia mtaa wa Mkondachi na kijijini kanda ya kati pia ligi hiyo
inatarajia kuendelea leo tarehe 5 mei 2015 katika viwanja vya Ludewa mjini
ikiwa ni mzunguko wa pili.
No comments:
Post a Comment