Wasanii wa iva youth group wakijiandaa kurekodi
Wasanii wa iva youth group wakijiandaa kurekodi
Wasanii wa iva youth group wakijiandaa kurekodi
Kikundi cha
sanaa kijulikanacho kwa jina la IVA YOUTH GROUP kilichoko wilaya ya Ludewa
katika mkoa wa Njombe kimeanza kutengeneza Filamu yao ambayo inamahadhi ya
wilaya ya Ludewa ikiwa ni Filamu ya kwanza tokea wilaya hiyo innzishwe.
Akiongea na
wanahabari wakati wa kurekodi Filamu hiyo katibu wa kikunchi hicho Bw.Leonard
Lukuwi alisema IVA YOUTH GROUP ni kikundi pekee kilichosajiriwa na baraza la
sanaa la Taifa(BASATA) kunafanya kazi mbalimbali za uelimishaji wa jamii katika
wilaya ya Ludewa na knapatikana Ludewa mjini
Bw.Lukuwi
alisema kuwa kikundi hicho kimekusanya wasanii mbalimbali katika kata na vijiji
vya wilaya ya Ludewa na kufikia wasanii 30 ambao wanafanya sanaa mbalimbali na
mpaka sasa wanaandaa Filamu ya kwanza ambayo itawatambulisha wanaludewa na
tamaduni zao.
Alisema kuwa
wilaya ya Ludewa inawasanii wenye vipaji vikubwa lakini wamesahaulika kutokana
na kukosa wadau ambao wangeweza kuwaibua na kuitangaza wilaya yao katika Taifa
na mataifa mengine ambayo yanafuatilia sanaa za Tanzania.
“vipaji vipo
Ludewa ila kinachokosekana na ufadhiri kwani mpaka sasa kikundi cha IVA hakina
mfadhiri na hakija wahi kupata ufadhiri wa aina yoyote licha ya kuwa ni kikundi
kikongwe kilianzishwa mwaka 2008 lakini kimekuwa kikitumiwa na mashirika katika
kuielimisha jamii katika mambo mbalimbali na sasa tumeamua kutengeneza filamu
hii kwa kujichangisha wasanii wenyewe ili tuweze kuinua uchumi wetu ndani ya
kundi”,alisema Bw.Lukuwi.
Filamu hiyo
inayotarajiwa kuzinduliwa mwezi juni mwaka huu ikiwa na wasasii chipukizi ambao
kwa mara ya kwanza wataanza kuonekana katika ulimwengu wa Filamu nchini hivyo amewaomba wadau mbalimbali kutoa michango kwa njia ya mpesa katika namba 0752 206242 ili kufanikisha filamu hiyo.
No comments:
Post a Comment