Katibu wa vijana wa CCM Bw.Menrad Mtega akitoka kuchimba shimo
Mwandishi wa mtandao huu Nickson Mahundi mwenye laba akiwa na mh.Mchilo katikati pamoja na muhandisi wa mradi huo Fredrick Mathia
Muhandisi wa mradi akiwajibika
Huyu ndyiye muhandisi wa mradi
Katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Lusiano Mbosa akiwajibika
Kazi na dawa diwani akichoma mahindi kwani njaa tayari
Wananchi
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameshauliwa kuendelea kudumisha dhana ya
kujitolea katika kazi mbalimbali ili kujiletea maendeleo haraka kwani mipango
ya Serikali ni ya muda mrefu hivyo huchelewa kutekelezwa kwa muda muafaka
kutokana na halihalisi ya bajeti ya Serikali kutokana na hali hiyo wananchi
yameanza kuchimba mashimo ya nguzo za umeme kuelekea kata ya Manda.
Hayo
yamesemwa leo na Diwani wakata ya Ludewa mjini kupitia chama cha mapinduzi
(CCM)Mh.Monica Mchilo wakati akifanya kazi uchimbaji wa mashimo ya kusimika
nguzo za nishati ya umeme katika mtaa wa Ngalawale ambapo wananchi kwa kushirikiana
na vingozi mbalimbali wameungana na wataalamu wa umeme kukamilisha zoezi hilo
la ujenzi wa njia ya umeme kuanzia Ludewa kijijini hadi kata ya Manda pembezoni mwa ziwa nyasa.
Mradi huo wa
Umeme ambao unafadhiriwa na Wakala wa nishati ya umeme vijijini(REA) kwa awamu
ya kwanza utaanzia Ludewa kijijini kuelekea maeneo ya Ngalawale,vijiji vya
Kimelembe,Nkomang’ombe,Luilo,Lifua na Kipangala na awamu ya pili utapita vijiji
vya Lihagule,Masasi,Kipingu,Ngelenge,Ilela,Nsungu,Igalu na Mbongo.
Mh.Mchilo
alisema wananchi wanapaswa kujitolea katika kazi mbalimbali ili kujiletea
maenteleo kwa haraka pale wanapoona tayari Serikali imeingiza mkoano wake kwani
kumekuwa na dhana potofu ya baadhi ya wanasiasa kuwakatisha tama wananchi
wakiwataka wabweteke na kuisubiri Serikali ifanye kila jambo hali ambayo si
sahihi.
“Nawapongeza
wananchi kwa kuamua kuanza kwa nguvu zenu kuliko mngeisubiri Serikali iwafanyie
kila jambo na huu ndio urithi aliyotuachia baba wa Taifa letu Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere na kama watanzania wangelitambua hili linalofanywa wilayani
Ludewa na kulitendea kazi basi kila kijiji na wilaya nchini kusingekuwa na
malalamiko ya kuilaumu Serikali”,alisema Mh.Mchilo.
Katibu wa
chama cha Mapinduzi (CCM)wilaya ya Ludewa Bw.Lusiano Mbosa alisema kuwa katika suala la maendeleo hakuna siasa hivyo
aliwataka wananchi kuendelea kujitolea kuchimba mashimo ya nguzo za umeme bila
kuwasikiliza wapinga maendeleo kwani umeme huo utawanufaisha wananchi na si
wapinga maendelea.
Bw.Mbosa
alisema kuwa ifike wakati siasa zikae kando kwani tayari Serikali kupitia
REA imeshatoa fedha za mradi huo wa
umeme hivyo kila mwananchi anapaswa kuhusika na uletwaji wa jambo hilo la
kimaendeleo ambalo litakinufaisha kizazi kilichoko na kijacho.
Aidha
msimamizi wa mradi huo wa ujenzi wa njia ya Umeme kutokea kata ya Ludewa hadi
kata ya Manda kutoka kampuni ya Power Magics Bw.Fredrick Mathia alisema katika
mradi huo anakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya ubovu wa barabara
katika msimu huu wa mvua hivyo magari yanayobeba nguzo kukwama katika tope.
Bw.Fredrick
alisema kuwa mpaka sasa kuna baadhi ya vijiji tayari nguzo zimeshafika lakini
bado kiasi kikuba cha nguzo hazijaletwa kwani mradi huo unatekelezwa kwa muda
wa miezi mitatu lakini kutokana na hali halisi utachelewa kukamilika kwa
wakati.
Alisema
ameshangazwa na umoja wa wananchi wa wilaya ya Ludewa kwa kujitolea kuchimba
mashimo ya nguzo za umeme tofauti na maeneo ambayo amewahi kufanya kazi hali
ambayo ni mfano wa kuingwa kwa wananchi wengine nchini.
No comments:
Post a Comment