Wazee
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameendelea kusisitiza kuwa wamechoshwa
na tabia iliyojengeka kwa wananchi wa wilaya hiyo ya kubadiri viongozi hasa kwa
upande wa nafasi ya ubunge kila kipindi cha uchaguzi hivyo wanamtaka mbunge wa
sasa wa jimbo hilo Deo Filikunjombe kuchukua fomu na kuendelea kuliongoza kwa
kipindi kingine cha miaka mitano.
Akiongea hivi
karibuni na mwandishi wa habari hii mwanasiasa mkongwe wilayani hapa ambaye
amewahi kuwa diwani wa kata ya Ludewa mjini na baadae kuwa mwenyekiti wa
Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kwa muda wa miaka 10 na kuamua kuachana na
siasa Mzee Hilali Nkwera alisema kuwa ni tabia iliyozoeleka kwa wananchi
kubadiri viongozi kila kinapofika kipindi cha uchaguzi hali ambayo inarudisha
maendeleo ya wilaya nyuma.
Mzee Nkwera
alisema katika historia ya wilaya ya Ludewa ni mbunge mmoja pekee ndiye
aliyewahi kudumu katika madara yake kwa muda wa miaka 25 ambaye ni hayati
Mathias Kihaule lakini tangia alipochukua utawala huo hayati Horace Kolimba
imekuwa ni mabadirishano ya kila kipindi hali ambayo ni mbaya kwa maendeleo
kwani mikakati ya kimaendeleo haiwezi kufanikiwa kwa muda wa miaka mitano.
Alisema kuwa
Filikunjombe ameanza kufanya maendeleo kwa kasi kubwa hivyo hapaswi kupingwa
zaidi ya kuungwa mkono kwa yale anayoyafanya kwani wananchi wa wilaya ya Ludewa
hawana haja na mtu mwingine wa kuliongoza jimbo hilo zaidi yake ambaye kupitia
Serikali ameweza kuibadiri wilaya kwa muda mfupi ambao amekuwa kiongozi.
“Sisi kama
wazee wa wilaya ya Ludewa hatuna haja ya mbunge mwingine kwani anayoyafanya
mtoto wetu Deo Filikunjombe tunayaona na ametuletea sifa kubwa nchini kuwa
kumchagua yeye ambaye ni mchapa kazi,wako vijana wanaokuja kutuomba tuwape
nafasi na tumewajibu wamuache mwezao aendelee na mipango aliyoianza kuitekeleza
ili wilaya ibadirike zaidi tofauti na zamani na nataka kuwaeleza wananchi kuwa
tumeamua kuacha tabia ya kubadirisha wabunge kila mwaka kwani tumeziona athari
zake za kurudi nyuma kimaendeleo”,alisema Mzee Nkwera.
Mzee Nkwera
alisema kuwa kila anapochaguliwa mbunge mwingine huanza na mipango yake ya
maendeleo lakini kabla haja maliza utekelezaji tayari kipindi cha miaka mitano
kinakuwa kimekwisha hivyo wilaya inabaki nyuma na kupitwa na wilaya za jirani
licha ya kuwa wilaya ya Ludewa ni moja kati ya wilaya tajiri nchini.
Nae
Bi.Gerewada Nyandoa alisema kwa upandewa wakina mama hawanashida na utendaji wa
Filikunjombe kwani ameweza kuwasaidia katika maendeleo ya ujenzi wa Zahanati
ambazo ni mkombozi kwa mwanamke wakati kabla ya ujenzi wa Zahanati hizo 3
wanawake walikuwa wakitembea umbali mrefu kwaajili ya kufuata huduma.
Bi.Gerewada
alisema hivi karibuni wazee wa kijiji cha Nsele kata ya Kilondo walitoa fedha
taslimu shilingi laki moja na kumkabidhi Filikunjombe ili aweze kujiandaa
kuchukua fomu ya kugombea Ubunge,fedha hizo ziliwakilisha wazee wote wa wilaya
ya Ludewa ambao wanadhamira ya kunufaika na kushuhudia maendeleo yanayoletwa na
kijana wao ambaye walimpigania kuchukua nafasi hiyo kwa manufaa ya wilaya na
Taifa.
Aidha Mzee
George Kilongo anayewakilisha wazee wa mwambao wa ziwa nyasa aliusifu utawala
wa Filikunjombe kuwa ni utawala wenye neema kwani ni mbunge ambaye ameweza
kutembelea vijiji vyake vyote vya ziwa nyasa ndani ya miaka mitano licha ya
kuwa kuna baadhi ya vijiji huwezi kufika kwa kutumia gari wala boti zaidi ya
kutembea kwa miguu kwa muda wa masaa 5 hali ambayo imewashangaza wananchi kuona
mbunge huyo akifika na msafara wake.
Mfano wa
vijiji hivyo vyenye mazingira magumu ya kufikika ni kijiji cha Liunji,Kimata na
Nkwimbili ambako hakuna mbunge ambaye aliwahi kifika lakini Filikunjombe
ameweza kuvitembelea na kutoa misaada ya Afya,Elimu na maji hali ambayo
imewafanya wananchi wa vijiji hivyo kuona kuwa mbunge huyo anapaswa kuendelea
kuiongoza wilaya ya Ludewa kwa muda mrefu ili kuendelea kuwasaidia wananchi.
Mzee Kilongo
alisema kila utawala unaneema zake kutokana na utendaji wa Filikunjombe pia
alielekeza pongezi kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Prof Jakaya
Mrisho Kikwete katika utawala wake kwa kuweza kuleta maendeleo katika vijiji
visivyo fikika kwa kupitia Filikunjombe.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment