Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

December 02, 2014

KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI CCM LUDEWA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUACHA KUHUBIRI SIASA.

Bw.Felix akiongea na waumini
 Bw.Haule akiimba pamoja na wanakwaya wa kanisa hilo

Waumini wakimsikiliza Bw.Felix Haule

Katibu wa Itikadi na uenezi CCM wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe Bw.Felix Haule amewataka viongozi wa Dini wilayani hapa kuacha kuhubiri siasa badala yake wahubiri neno la Mungu na kuliombea amani taifa ili Tanzania iendelee kuwa amani na viongozi waadili na wenye kumpendeza Mwenyezi Mungu.

Bw.Haule aliyasema hayo hivi karibuni wakati wa harambee ya ukarabati wa kanisa la Anglikani Mtakatifu Andrea kijiji cha Kipangala kata ya Luilo wilayani Ludewa ambapo yeye alialikwa kuwa mgeni rasmi wa harambee hiyo.

Katika harambee hiyo kiasi cha shilingi 337000 zilikusanywa ambapo alitoa ahadi ya kulipiga langi kanisa lote ikiwa ni mchango wake katika harambee hiyo kwani awali kanisa hilo lilihitaji kiasi cha shilingi milion moja ili kufanikisha ukarabati mzima ikiwemo na rangi ya kani sa lote.

Bw.Haule alisema kuna baadhi ya viongozi wa Dini wameanza kuhubiri siasa wakisahau kazi yao hali ambayo inawakera baadhi ya waumini wenye nia ya kulisikiliza neno la Mungu ambalo hawawezi kulipata wakiwa mitaani hivyo ni vyema kuhubiri amani ya taifa letu ili Tanzania iendelee kuwa nchi ya amani na kuwa mfano kwa mataifa mengine.

“Nawaomba viongozi wangu wa Dini tuache kuhubiri siasa kwa waumini wetu badala yake tuliombee taifa amani na kuwa na viongozi waadirifu ambao wanamuogopa mwenyezi Mungu kwani kuna baadhi ya viongozi wa dini wameacha wajibu wao wameingia huku kwetu kwenye mambo ya siasa haya mtuachie wanasiasa”,alisema Bw.Haule.

Baba Padre John Haule ambaye ni Padre wa kanisa hilo alimshukuru katibu wa itikadi na uenezi kwa machango wake mkubwa wa ukarabati wa kanisa hilo ambalo limekuwa likitafuta ufadhiri kwa muda mrefu bila ya mafanikio na hatimaye kupata mtu ambaye ameweza kuchangisha watu na kutoa rangi ya kutosha kanisa lote.

Padre Haule alisema kuna baadhi ya viongozi wa dini wamekuwa na tabia za kuwaingilia wanasiasa katika mambo yao hali ambayo si sahihi ni bora wakaachana na mambo ya kidini na kujikita katika suala la siasa.

Mwisho.

No comments: