Mh.Faraja Mlelwa akiongea na wananchi wa kijiji cha Kiyombo kata ya Mlangali wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe
Mh.Mlelwa akifungu Darubini kushoto kwake ni ofisa mtendaji wa kata ya Mlangali Bw.Venant Lupagalo
Mh.Mlelwa akimkabidhi Darubini mganga mkuu wa Zahanati ya Kiyombo Bw.Maneno Mlowe
Mh.Mlelwa akipongezwa na mwenyekiti wa kijiji cha Kiyombo Bw.Manaseta Tamaambele
Hii ndiyo Darubini aliyoitoa Mh.Faraja Mlelwa
umati wa wananchi uliofulika katika kijiji cha kiyombo wakimsikiliza Mh.Mlelwa
wananchi wa kijiji cha kiyombo wakimskiliza Mh.Mlelwa katika mkutano
Wananchi wakimpongeza Diwani Mlelwa kwa kutoa Darubini
Wananchi wa kijiji cha Kiyombo kata ya Mlangali wilaya ya
Ludewa mkoani Njombe wanaandaa siku maalum ya kufanya sherehe ya kumpongeza
diwani wa kata hiyo kupitia chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA)
Mh.Faraja Mlelwa kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya kata hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na wananchi hao katika mkutano wa
hadhara uliofanyika kijijini hapo wakati Diwani huyo akikabidhi Darubini katika
Zahanati ya kijiji cha Kiyombo ikiwa ni moja ya ahadi zake alizozitoa wakati
akigombea nafasi hiyo hivyo kuwafanya wananchi hao kuona mchango wake katika
jamii.
Akiongea kwa msisitizo katika mkutano huo mwananchi mmoja aliyejitambulisha
kwa jina la Deogras Mtitu alisema imefika wakati Mh.Mlelwa anapaswa kuandaliwa
siku maalum ya kumpongeza kwani amefanya kazi mbalimbali kwa kushirikiana na
wananchi akitumia fedha zake kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.
Bw.Mtitu alisema ndani ya kijiji cha Kiyombo ametoa vioo 48
kwaajili ya ujenzi wa ofisi ya kijiji,ametoa fedha kwaajli ya kutengeneza
madawati katika shule ya msingi na hatimaye kununua Darubini ambayo itawasaidia
wananchi wa vijiji vyote vya kata ya mlangali katika kupima afya zao.
“ni lazima tumuandalie siku ya kumpongeza kwa haya
tunayoyaona kwani anafanya mambo mengi bila kujari itikadi za
kisiasa,ukiangalia ndugu mwandishi kule kitongoji cha madindo tayari wana maji
ya bomba kutokana nay eye kwa kushirikiana na viongozi wengine wa vijiji lakini
hasa yeye amekuwa mbunifu wa mambo mengi kutokana na elimu yake kubwa
aliyonayo”,alisema Bw.Mtitu.
Naye Bi.Magreth Mchilo alisema awali waliweza kuazima
Darubini kutoka kijiji jirani cha Ligumbilo lakini wagonjwa walio wengi
waliweza kusafiri umbali wa kilomota zaidi ya 15 hadi hospitari ya Lugarawa ili
kupima afya zao hivyo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa kijiji hicho na vile
vya jirani kuwa na Darubini hiyo ya kisasa.
Licha ya kuwa na Diwani huyo kufanya mambo mengi ndani ya
kata ya Mlangali lakini Bi.Magerth alimuomba Mh.Mlelwa kuwasaidia katika ujenzi
wa shule ya msingi katika kitongoji cha Mtemaruchi kijijini hapo.
Alisema shule hiyo ni ya muda mrefu lakini hadi sasa haku
kinachoendelea licha ya kuwa wananchi hao walijitolea nguvu zao katika kuanza
ujenzi lakini hakuna jitihada zinazoendelea hali inayopelekea watoto wengi
kukua bila ya kujua kusoma na kuandika.
Bi.Magreth alisema kuna hatari ya kuzalisha vibaka kwani
baadhi ya watoto wanaolazimishwa kwenda kusoma umbali mrefu huishia vichakani
na kujifunza mambo yasiyofaa hivyo kama shule hiyo itakamilika kizazi hicho
kinachokua bila kusoma na kuandika kitatoweka na kitongoji hicho kitapata
maendelo kwa kuzalisha wasomi.
Aidha Diwani huyo aliwataka wananchi kushirikiana katika
kuleta maendeleo katika maeneo yao pasipo kuisubiri Serikali kwani hata yeye
amekuwa mstari wa mbele kujitolea kwenye maendeleo bila ya kujari itikadi za
kisiasa kwa kufanya hivyo kila kijiji kitainuka kiuchumi.
Mh.Mlelwa aliwataka wananchi kuacha kulalamika kwani kuna
baadhi ya watu wamekuwa wakigomea shughuri za maendeleo kwa kisingizio kuwa wao
ni wanachadema kwa maana hiyo hawawezi kufanya kazi za maendeleo zilizopangwa
na watendaji wa CCM.
Alisema maendelo ya kijiji si ya CCM bali ni ya wananchi
wote pia chama cha demokrasia na maendeleo(CHADEMA) kingependa kuona wananchi
wenye maendeleo ya kweli na si umaskini ulokithiri kutokana na kushindwa
kufanya kazi kwa kuitegemea Serikali ya ccm.
Hata hivyo aliwasifu wananchi hao kwa kumuunga mkono katika
kazi mbalimbali za kimaendeleo anazozifanya katika kata yake ambapo aliwataka
kuendelea na ushirikiano huo hata katika uchaguzi wa Serikali za mitaa
unaotarajiwa kuwanyika mwishoni mwaka huu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment