Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

October 07, 2014

CHAMA CHA WALIMU LUDEWA CHAIOMBA SERIKALI KUWONDOLEA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WALIMU.

Bw.Mvanginye ambaye ni makamu wa katibu chama cha walimu wilayani Ludewa



Chama cha walimu wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe (CWT)kimeitaka Serikali wilayani hapo na nchini kuziondoa changamoto zinazowakabili walimu ili kurahisisha utendaji wa kazi hasa kwa walimu wanaoishi jijijini kwani kumekuwa na mazingira magumu zaidi.


Akisoma risala kwa mgeni rasmi jana katika kilele cha siku ya walimu Duniani iliyofanyika kiwilaya katika kata ya Lupanga makamu katibu wa chama hicho wilaya ya Ludewa Bw.Florian Mvanginye alisema walimu wilayani hapa wamekuwa wanakumbwa na changamoto nyingi ambazo zinapelekea ugumu wa utendaji kazi.


Kizitaja moja ya changamoto hizo Bw.Mvanginye alisema ni pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kuwataka walimu kulipia kodi za nyumba wanazoishi katika vijiji wilayani hapa hali ambayo imekuwa ni tatizo kubwa kwa walimu hao kutokana na ugumu wa maisha katika maeneo yao ya kazi.


Alisema walimu wamekuwa wakikatwa michango mingi kutokana na uwingi wao kwani wako ambao hutumia fedha nyingi za nauli wanapokuja mjini kufuata mishahara hali ambayo inawarudisha nyuma kimaendeleo hivyo nyumba wanazoishi maeneo ya shule ingekuwa kama motisha kwa walimu hao.


Bw.Mvanginye alisema walimu wamekuwa wakifanya kazi muda mwingi bila ya malipo ya ziada hvyo kuimba Serikali kupunguza muda wakazi badala ya 10.30 wawe wanafanya kazi mwisho saa 9.30 na muda unaobakia utumike kwa kuandaa masomo ya siku iayofuata.


“Ndugu mgeni rasmi walimu tumekuwa ni watu wa kudharaulika kutokana na mazingira tunayofanyia kazi ikumbukwe hakuna aliyefanikiwa katika maisha bila ya mwalimu kwani hata muasisi wa taifa hili alikuwa mwalimu na mwalimu aliheshimiwa lakini kwa sasa imekuwa tofauti na awali,tunaomba kuthaminiwa kwani tunamchango mkubwa katika jamii”,alisema Bw.Mvanginye.


Alisema idadi ya walimu vijijini ni ndogo mno ukilinganisha na wanafunzi wanaotakiwa kufundishwa hivyo aliiomba Serikali kuajiri walimu wengi ili waweze kwenda sambamba na mahitaji.


Aidha mgeni rasmi wa sherehe hizo ambaye pia ni katibu tarafa wa tarafa ya Mlangali Bw.Ezekiel Magehema alisema Serikali iko mbioni kurekebisha changamoto zinazowakabili walimu nchini.


Kuhusu kutozwa kodi katika nyumba Bw.Magehema alisema mpaka sasa Halmashauri ya Ludewa inajaribu kuliangalia hilo hivyo vikao bado vinaendelea kwa kufanya tathmini ya nyumba zote za Serikali na zoezi likisha kamilika basi majibu sahihi yatatolewa kuwa nni kifanyike ili walimu waendelee na utaratibu wa kuishi katika nyumba hizo.


Mwisho.


No comments: