Chama cha
walimu wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe (CWT)kimeitaka Serikali wilayani
hapo na nchini kuziondoa changamoto zinazowakabili walimu ili kurahisisha
utendaji wa kazi hasa kwa walimu wanaoishi jijijini kwani kumekuwa na mazingira
magumu zaidi.
Akisoma risala
kwa mgeni rasmi jana katika kilele cha siku ya walimu Duniani iliyofanyika
kiwilaya katika kata ya Lupanga makamu katibu wa chama hicho wilaya ya Ludewa
Bw.Florian Mvanginye alisema walimu wilayani hapa wamekuwa wanakumbwa na
changamoto nyingi ambazo zinapelekea ugumu wa utendaji kazi.
Kizitaja moja
ya changamoto hizo Bw.Mvanginye alisema ni pamoja na Halmashauri ya wilaya ya
Ludewa kuwataka walimu kulipia kodi za nyumba wanazoishi katika vijiji wilayani
hapa hali ambayo imekuwa ni tatizo kubwa kwa walimu hao kutokana na ugumu wa
maisha katika maeneo yao ya kazi.
Alisema walimu
wamekuwa wakikatwa michango mingi kutokana na uwingi wao kwani wako ambao
hutumia fedha nyingi za nauli wanapokuja mjini kufuata mishahara hali ambayo
inawarudisha nyuma kimaendeleo hivyo nyumba wanazoishi maeneo ya shule ingekuwa
kama motisha kwa walimu hao.
Bw.Mvanginye
alisema walimu wamekuwa wakifanya kazi muda mwingi bila ya malipo ya ziada hvyo
kuimba Serikali kupunguza muda wakazi badala ya 10.30 wawe wanafanya kazi
mwisho saa 9.30 na muda unaobakia utumike kwa kuandaa masomo ya siku iayofuata.
“Ndugu mgeni
rasmi walimu tumekuwa ni watu wa kudharaulika kutokana na mazingira
tunayofanyia kazi ikumbukwe hakuna aliyefanikiwa katika maisha bila ya mwalimu
kwani hata muasisi wa taifa hili alikuwa mwalimu na mwalimu aliheshimiwa lakini
kwa sasa imekuwa tofauti na awali,tunaomba kuthaminiwa kwani tunamchango mkubwa
katika jamii”,alisema Bw.Mvanginye.
Alisema idadi
ya walimu vijijini ni ndogo mno ukilinganisha na wanafunzi wanaotakiwa
kufundishwa hivyo aliiomba Serikali kuajiri walimu wengi ili waweze kwenda
sambamba na mahitaji.
Aidha mgeni
rasmi wa sherehe hizo ambaye pia ni katibu tarafa wa tarafa ya Mlangali
Bw.Ezekiel Magehema alisema Serikali iko mbioni kurekebisha changamoto
zinazowakabili walimu nchini.
Kuhusu kutozwa
kodi katika nyumba Bw.Magehema alisema mpaka sasa Halmashauri ya Ludewa
inajaribu kuliangalia hilo hivyo vikao bado vinaendelea kwa kufanya tathmini ya
nyumba zote za Serikali na zoezi likisha kamilika basi majibu sahihi yatatolewa
kuwa nni kifanyike ili walimu waendelee na utaratibu wa kuishi katika nyumba
hizo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment