Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

September 01, 2014

FILIKUNJOMBE AWATAKA WANASIASA KUACHA TOFAUTI ZA KISIASA KATIKA KULETA MAENDELEO KWA WANANCHI

 Jiwe la msingi alilozindua Filikunjombe katika kata ya Mlangali wilayani Ludewa kata ambayo Diwani wake anatoka chama cha CHADEMA

Filikunjombe akishirikiana na wananchi kushusha tank la maji ambalo alilitoa kwa wananchi wa kitongoji cha Madindo kata ya Mlangali ambako walimuomba ili kulinusuru tatizo la maji
 Filikunjombe akishiriki kuchimba mtaro wa maji na wananchi wa Mlangali
hiki ndicho chanzo cha maji ya Madindo
Diwani wa kata ya Mlangali kupitia Chadema Bw.Faraja Mlelwa akimtwisha Ndoo ya maji Filikunjombe baada ya mradi huo kukamilika





Mbunge wa jimbo la Ludewa katika mkoa wa Njombe Mh.Deo Filikunjombe amewataka wanasiasa nchini kutoingiza itikadi za kisiasa katika kazi za kimaendeleo ambapo alisema wananchi hawana haja na maneno ya kisiasa kwa kipindi hiki bali ni maendeleo katika maeneo yao.

Filikunjombe aliyasema hayo hivi karibuni wakati akizindua mradi wa maji katika kitongoji cha Madindo kata ya Mlangali wilayani Ludewa ambaoulianzishwa na wananchi wenyewe kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji cha Mlangali na kusaidiwa na Faraja Mlelwa ambaye ni Diwani wa kata hiyo kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).

Alisema wanasiasa wamekuwa na kasumba ya kukwamisha juhudi za Kimaendeleo pale wanapoona kiongozi tofauti na chama chake anafanya kazi za kimaendeleo kwa wananchi katika eneo lake kitu ambacho si sahihi kwani wakati wa kupiga siasa ni kipindi cha kampeni na si kipindi hiki ambacho kila mwanasiasa anatambua anatekeleza ilani ya CCM.

 Alisema ifike wakati wanasiasa wafanye kazi ili kuwaletea wananchi maendeleo na si kurumbana kwa kauli zisizo za msingi na manufaa kwa wananchi kwani kama wanasiasa wataacha kuingiza siasa katika utendaji kazi basi taifa litasonga mbele kwa haraka zaidi kutokana na Ilani za Chama Cha Mapinduzi kuwa nzuri na zinazotekelezeka kirahisi.

"nimependa utendaji wa Diwani Faraja ingawa anatoka chama tofauti na ninachotoka mimi lakini hata yeye anatambua anatekereza ilani ya Chama changu na laiti kama wanasiasa wote tungelikuwa na ushirikiano wa kuwaletea wananchi maendeleo kwa kutatua kero zao kama hivi basi hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kumuonesha kidole mwenzie",alisema Filikunjombe.

Katika mradi huo Filikunjombe aliweza kuchangia matenki mawili yenye ujazo wa lita 1000 za maji ambayo wananchi kupitia Diwani wao walimuomba mbunge huyo kuwasaidia kutokana na kukwama kuendelea kusambaza maji kwa wananchi wengine.

Aidha Diawani wa kata hiyo Mh.Faraja Mlelwa  kupitia chama cha demokrasia na maendeleo alimshukuru Mh.Filikunjombe kwa kuwa msikivu kwa wananchi bila kujali itikadi ya vyama vyao kwa kutoa msaada amabo aliombwa na Diwani huyo na kushiriki na wananchi katika kazi za kimaendeleo.

Mh.Mlelwa alisema wananchi wamekuwa na imani na Mbunge wao kwani kila wanapopatwa na tatizo Filikunjombe huungana nao katika kutatua tatizo hilo hivyo kupitia ushirikiano anaoutoa kwa wananchi wake wananchi hawajudii kuchagua Mbunge huyo kuwa mtetezi wao.

Alisema imefika wakati wanasiasa wanatakiwa kushirikiana katika kuleta maendeleo kwa wananchi na si kurumbana kwani kiu ya wananchi ni maendeleo na si vinginevyo kama baadhi ya wanasiasa wanavyofikiri.

No comments: