mbwa aliyesababisha mauti ya marehemu Ibrahimu Faraja Chipungahelo
Mtoto mmoja
alifahamika kwa jina la Ibrahim Faraja Chipungahelo(9) aliyeishi mtaa wa ibani
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wmwanafunzi wa shule msingi Kimbila
darasa la tatu amevamiwa na Mbwa wakali ambao walimwangusha chini na kuanza
kumtafuna hadi kufa papo hapo wakati akijitahidi kuwaokoa watoto wenzake ambao
walizongwa na mbwa hao wawili.
Shuhuda
aliyekuwa katika tukio hilo ambaye anafahamika kama Mama haule akisimulia mkasa
huo uliotokea jana maeneo ya Ikulu alisema watoto hao walikuwa atano ambapo
marehemu na wenzake walikua wakienda nyumbani kwa babu yao kuchuma matunda aina
ya mapera alipokutwa na mkasa huo.
Mama Haule
alisema Marehemu Ibrahimu na watoto wenzie ilikuwa ni kawaida yao kupita katika
maeneo ya Ikulu ya wilaya ya Ludewa wakielekea kwa babu yao lakini eneo hilo la
Ikulu limekuwa hatari kutokana na mwananchi mmoja ambaye ni Bosco Lingalangala
kununua nyumba moja ambayo amefuga mbwa wawili wakali wasio kuwa na uangalizi
wakutosha.
Alisema
marehemu akiwa anapita ghafra walianza kuwavamia ndipo alipo jitahidi kuwaokoa
wenzie wadogo zaidi na mbwa hao kumkamata na kuanza kumlalua maeneo mbalimbali
ya mwili wake ambapo wenzie walitimua mbio na kumuacha akitafunwa na mbwa hao
wakali.
“Nilisikia
mtoto akilia nilipofuatili kwakua naishi jirani na nyumba ya Bw.Lingalanga
nikaona watoto wadogo wanakimbia nikawauliza kulikoni wakanijibu wenzetu
kakamatwa na mbwa nilipofika eneo la tukio niliwakuta Mbwa wawili wakiwa
wamemlaza chini mtoto wakimtafuna
nilipojaribu kusogea karibu mbwa hao walikuwa wakali sana ndipo kakimbia kuomba
msaada kwa askari polisi akaja na silaha alipo jaribu kuwalenga wakakimbia
lakini walishakuwa wamemuua na wanamla”,alisema mama Haule.
Mama Haule
alisema alivyojaribu kumuinua marehemu alikuta ameharibiwa vibaya sehemu za
siri na kuliwa misuri yote ya mapaja na tayari alikwisha poteza uhai hivyo kwa
kusaidiana na wasamalia wema waliuchukua mwili wake na kuupeleka hospitari ili
uhifadhiwe.
Aidha
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa
Njombe ASP Furgency Ngonyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo
alisema tayari hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa dhizi mmiliki wa mbwa
huyo kwani tayari kijana wa mmiliki ambaye alikabidhiwa kuwahudumia mbwa hao
yuko chini ya ulinzi huku taratibu nyingine zikiendelea.
Kamanda
Ngonyani alisema wakati taratibu za jeshi hilo zikiendelea amewataka wananchi
wa mkoa wa Njombe kuwa waangalifu hasa wanaofuga mbwa wawe na tabia ya
kuwafunga nyakati za mchana ili kuepusha ajali zisizo za lazima kama tukio
hili.
Naye ofisa
mifugo msaidizi Bw.Simon Haule alisema tayari mbwa mmoja ameshauawa kwa kupigwa
risasi baada ya tukio hilo lakini mwingine amekimbia hajulikani aliko hivyo
juhudi za kumsaka ili naye auawe zinaendelea.
Bw.Haule
alisema mmiliki wa mbwa hao amekuwa ni mzembe kwani hajawatibu kwa muda wa
miaka miwili mpaka sasa hivyi kuna uwezekano mkuwa kuwa walikuwa wanamagonjwa
ndicho chanzo cha kufanya tukio hatari kama hilo ambalo limesababisha kukatisha
uhai wa mtoto.
Bw.Haule
amewataka wananchi wilayani hapa kuacha tabia ya kutembea usiku kwa mbwa mmoja
bado haja uawa na hajulikani aliko licha yakuwa juhudi za kumtafua zinaendelea
kwa anaweza kusababisha madhara mengine wakati wowote kama akikutana na
binadamu kutokana na kuwa ameshaonja damu ya mtu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment