FILIKUNJOMBEA AVUTIWA NA DIWANI WA CHADEMA KUTEKELEZA ILANI YA CCM ,AMPA ZAWADI YA KOFIA YA CCM
Mradi huu umeanzishwa na diwani wa Chadema kata hiyo |
Filikunjombe akiongea kabla ya kumzawadia kofia diwani Mlelwa |
Mbunge Filikunjombe akizunguma baada ya kumzawadia kofia yake diwani wa kata ya Mlangali Faraja Mlelwa |
MBUNGE
wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amempongeza diwani wa kata ya
Mlangali kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo ( chadema )
Faraja Mlelwa kwa hatua yake ya kuweka itikadi ya vyama kando
na kushiriki katika utekelezaji wa ilani ya CCM.
Kuwa
hatua ya diwani huyo kushughulikia kero ya maji kwa kuwafikishia
maji ya bomba wakazi wa kitongoji cha Madindu kata ya Mlangali ni
jambo njema na ni mfano wa kuingwa kwa wapinzani wengine ambao
siku zote wao ni mabingwa wa kuhamasisha wananchi kutoshiriki
maendeleo.
Akizungumza
jana wakati wa uzinduzi wa mradi huo wa maji ambao umegharimu
zaidi ya milioni 4.7 na diwani huyo kuchangia kiasi cha Tsh 500,000
kuunga nguvu kazi za wananchi ,mbunge Filikunjombe alisema kuwa
uamuzi wa kuibua mradi huo ni uamuzi wa kizalendo .
Kwani
alisema wazo hilo la kuwa na mradi wa maji ili kuondoa kero ya maji
katika kitongoji hicho ilibuniwa na mwenyekiti wa serikali ya
kijiji pamoja na diwani huyo japo awali mradi wa maji katika
eneo hilo kwa kuwatumia wataalam wa Halmashauri mradi huo wa
maji ungetumia zaidi ya Tsh milioni 80.
"
Nimeelezwa kuwa walikuja wataalam wa maji kutoka Halmashauri ya
Ludewa na kuchora mchoro wa mradi huo na makisio ya mradi mzima na
ili watu waweze kupata maji ilikuwa ni Tsh milioni 80 fedha ambazo
zisingepatikana kwa sasa na hivyo wananchi wangekuwa hawana
huduma hii ya maji ....mimi huyu diwani si wa chama changu ni
mpinzani ila katika hili namuunga mkono "
Pia
alisema ataendelea kuungana na diwani huyo kuwasaidia wananchi
wake kwani diwani Mlelwa ameonyesha kutekeleza ilani ya CCM na
mbali ya kuwa yeye kama mbunge na diwani huyo vyama tofauti bado
ameamua kumwalika kuzindua mradi huo.
Filikunjombe
alisema kuwa mahitaji mengine ambayo yanahitajika katika mradi huo
likiwemo tenki ya kuhifadhia maji la lita 5000 atalinunua pamoja
na kuanzisha ujenzi wa tenki la kudumu ambalo litahifadhi maji
zaidi ya lita 10,000
Hivyo
alisema kuwa kazi ya ujenzi wa tenki hilo anataraji kuongoza
mwenyewe siku ya tarehe 17 mwezi huu kwa kufika kijijini hapo
kushiriki shughuli ya ujenzi wa tenki hilo kama sehemu ya kuunga
mkono jitihada hizo za diwani na wananchi katika kujiletea
maendeleo.
Hata
hivyo alisema kuwa mahitaji ya wananchi hao ambao walikuwa na kero
kubwa ya maji si serikali tatu ama katiba mpya bali mahitaji yao
yalikuwa ni maji na kero nyingine zinazowakabili .
Diwani
wa kata hiyo Bw Mlelwa mbali ya kumpongeza mbunge huyo kwa
kuahidi kuwaunga mkono katika ujenzi wa tenki hilo bado alisema
ataendelea kufanya kazi kwa karibu na mbunge huyo bila kutangulia
itikadi za chama chake .
No comments:
Post a Comment