SERIKALI WILAYANI RUNGWE NA KYELA ZATEKETEZA BIDHAA HARAMU ZA TSH,MIL.90
SERIKALI
wilayani Rungwe mkoani Mbeya imeteketeza kwa kuvichoma moto vipodozi venye
viambata vya sumu pamoja na pombe haramu za viroba tani 380 vyenye thamani ya
Tsh mil,80 vilivyokuwa vinaingizwa nchini kutoka Malawi na
wafanyabiashara wasio waaminifu kwa lengo la kujiingizia kipato huku wakiharibu
maisha ya watanzania waliokuwa wakizitumia pombe hizo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana mara baada ya uchomaji huo mkuu wa wilaya hiyo
Chrispin Meela alisema kuwa vipodozi na pombe hizo walizikamata katika
operesheni iliyofanyika mwanzoni mwa mwaka 2013 hadi mwezi april mwaka 2014
katika msako ulioendeshwa na kikosi kazi cha kamati ya ulinzi na usalama pamoja
na maafisa wa TFDA na TRA na kufanikisha zoezi hilo.
Alisema
wafanyabiashara wasio waaminifu wamekuwa wakivusha vipodozi hivyo kutoka nje ya
nchi kwa njia za panya zilizopo mipakani, na kwa upande wa pombe kali za viroba
toka Zambia na Malawi wamekuwa wakipitisha kwenye mpaka wa Kasumulu boda kwa
njia za panya zilizogunduliwa kuwa ni 32 na kuzipeleka mikoani kwa ajiri ya
kuziuza huku wakifahamu kuwa bidhaa hizo ni haramu na hazijadhibitiswa.
Meela aliongeza
kuwa amewaagiza askari wa usalama barabarani wawe makini kukagua bidhaa hizo
ambazo kwa sasa aina mama wamekuwa wakipakatia mithiri ya mtoto mchanga na kuwa
bidhaa hizo zimekwisha poteza maisha ya watanzania wengi na wengine wamekwisha
haribikiwa hivyo Taifa limekuwa likipoteza nguvu kazi hasa kwa vijana.
Aliongeza kuwa
kwa sasa watatumia sheria za TRA pindi watakapo kamata bidhaa hizo watataifisha
bidhaa pamoja na gari badara ya ile sheria ya TFDA ya kutoza faini pindi wanapo
kamata bidhaa haramu ambayo haijadhibitiswa na kuwa wameamua kufanya hivyo ili
kuhakikisha bidhaa hizo hazitumiki tena na badala yake zitumike bidhaa za
kitanzania ambazo zimedhibitishwa na shirika la viwango nchini TBS.
Kwa upande
wa wilaya ya Kyela Serikali ya wilaya hiyo imeteketeza na kuchoma moto bidhaa
hizo zenye thamani ya Tsh,mil,1.2 huku mkuu wa wilaya hiyo Magret Malenga
akitoa msisitizo kwa vijana kuacha kuzitumia bidhaa hizo kwa madai kuwa
zinamadhara makubwa yanayoweza kuwapata pindi watumiapo.
Malenga alisema
kuwa bidhaa zingine bado hazijachomwa kwa kuwa bado zina kesi ambazo
zinaendelea mahakamani na kwamba ameiagiza idara husika kufanya doria maeneo
yote hasa katika njia hizo 32 za panya zinazotumika kuvushia bidhaa hizo na
watakapo mkamata mtu na bidhaa hizo wataitahifisha na mwenyebidhaa atafikishwa
mahakamani.
Meneja wa
mamlaka wa chakula na dawa kanda ya kusini Rodney Alananga alisema kuwa baada
ya kukithiri kwa uingizwaji wa bidhaa hizo alitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa
Abbas kandoro ambaye aliitisha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na kuwaagiza
wakuu wa wilaya kuanzisha msako huo ambao umezaa matunda na uigizwaji na uuzaji
wa bidhaa hizo umepungua kwa asilimia 80.
Alananga alisema
kuwa TFDA imewapa meno kamati za ulinzi na usalama zilizo chini ya wakuu wa
wilaya kwa kushirikiana na maafisa wa TRA kuhakikisha wanaendelea na zoezi hilo
ili kuhakikishwa wanafanikiwa kuzitokomeza bidhaa hizo huku watanzania
wakiendelea kuwa salama kwa kuzitumia bidhaa zilizo salama zilizodhibitiswa na
shirika la viwango n chini yaani TBS.
Mwisho.
0767269996
No comments:
Post a Comment