Akiongea na tovuti hii Sokoni Hapo Baadhi ya Wafanatbiashara Hao Wamesema Kuwa Kwa Muda Mrefu Wamekuwa Wakikabiliwa na Changamoto ya Ukosefu wa Huduma ya Umeme na Maji Hali Inayosababisha Soko Hilo Kuwa Chafu.
Wakielezea Suala la Usafi Ndani ya Soko Hilo Wamesema Kuwa Licha ya Kutoa Fedha Kwa Ajili ya Kuzoa Taka Lakini Bado Zoezi la Kuzoa Taka Hizo Limekuwa Likichelewa na Kusababisha Mlundikano wa Taka na Harufu Mbaya Inayohatarisha Afya za Wafanyabiashara na Wateja Wanaofika Sokoni Hapo Kwa Ajili ya Kujipatia Mahitaji Yao.
Isakwisa Kilagane ni Makamu Mwenyekiti Wa Soko Hilo Amekiri Kuwepo Kwa Changamoto Hizo na Kusema Kuwa Tayari Taarifa Wamezifikisha Katika Ofisi ya Uongozi wa Halmashuri ya Mji wa Njombe na Kujibiwa Kuwa Changamoto Hizo Zitafanyiwa Kazi Lakini Hadi Sasa Hakuna Hatua Yoyote Inayochukuliwa Kumaliza Tatizo Hilo.
No comments:
Post a Comment