Wachungaji mbalimbali wa makanisa ya Kirutheli wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Ludewa
Maaskofu wakiwa na mkuu wa wilaya ya Ludewa katika picha ya pamoja
MKUU wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Solomon
Madaha amezitaka asasi za kidini kuwekeza katika maeneo mbalimbali wilayani
Ludewa ili kuweza kujiongezea uwezo wa kujiendesha kwani bila kufanya hivyo
asasi hizo zinaweza kuwa tegemezi kwa wafadhiri.
Bw.Madaha aliyasema hayo katika kanisa la
Kirutheli wilayani Ludewa ambapo wajumbe mbalimbali wa kanisa hilo kutoka
wilaya za mkoa wa Njombe wanahudhuria mkutano wa siku tatu wa kiroho ambao
umeandaliwa na uongozi wa jimbo la mkoa huo.
Alisema kuokana na hali halisi ya wilaya
ya Ludewa kwa sasa ambapo Mei 2014 ujenzi wa viwanda vya chuma katika mgodi wa
Liganga na ufuaji umeme katika majimbo ya Mchuchuma unatarajia kuanza asasi za
kidini hazina budi kujipanga katika kuwekeza maeneo ya Ardhi ili kuweza
kujitengemea zaidi katika kuhudumiaa jamii.
Bw.Madaha alilishukuru kanisa la kiinjili
la Kilutheri na makanisa mengine kwa kuwa bege kwa bega katika kushirikiana na
Serikali katika kuihudumia jamii hasa maeneo ya Elimu,Afya na ujenzi wa maadili
miongoni mwa vijana ambao wamekuwa wakimomonyoa maadili kila siku.
“kutokana na ujio wa wawekezaji wilayani
Ludewa tunatarajia kuwa na watu wengi ambao watafanya kazi katika miradi ya
Liganga na Mchuchuma hivyo ninyi kama asasi za kidini ni vema mngeanza kuwekeza
katika sekta mbalimbali ili kuacha utegemezi kwa wafadhiri,kwa kufanya hivyo
mtaongeza ajira kwa waamini wenu na kuwa na maisha bora”,alisema Bw.Madaha.
Alisema wananchi wa wilaya ya Ludewa
wameanza kuandaliwa katika kutumia fulsa zilizopo ili kunufaika na miradi hiyo
mikubwa hivyo hata asasi za kidini zote
nchini zinakaribishwa kuwekeza wilayani Ludewa kwani kwa kuchelewa kwao kushika
maeneo ya uwekezaji asasi zitashindwa kufaidika na fulasa za migodi,
Kuhusiana na suala la maambukizi ya gonjwa
la ukimwi Mkuu huyo wa wilaya aliwataka viongozi wa dini kuhubiri zaidi maadili
na utii wa amri za mwenyezi Mungu kwani mpaka sasa mkoa wa Njombe unaongoza kwa
14.5% ya ukimwi kwa Tanzania ikifuatiwa na mikoa mingine.
Bw.Madaha alisema kama waumini
watahubiliwa kuacha dhami ya zinaa basi sifa hiyo mbaya ya mkoa wa Njombe
kuongoza katika suala la maambukizi ya ukimwi litakwisha na ongezeko la watoto
yatima na wa mtaani litapungua kwa kiasi kikubwa.
Alisema suala la maambukizi ya ukimwi
linasababishwa na mmomonyoko wa maadili kuanzia ngazi ya familia hivyo kuongoza
katika suala hilo sio sifa nzuri hivyo kila kiongozi wa Dini aliyoko mkoa wa
Njombe anapaswa kulitilia mkazo suala hilo ili kutoka katika sifa hiyo mbaya
nchini.
No comments:
Post a Comment