Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

August 28, 2013

MZAZI AMFUKIA MTOTO WAKE NDANI YA SHIMO MAKAMBAKO NJOMBE.



ACP Fulgency Ngonyan Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Amethibitisha Kutokea kwa Matukio Hayo.
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Linawashikilia Watu Wawili Maria Kilasi na Charles Mbata Wakazi wa Wilaya ya Njombe Kwa Tuhuma Tofauti ,Ambapo Maria Kilasi Anatuhumiwa Kutupa Mtoto Mchanga Ndani ya Shimo na Kisha Kumfukia na Kusababisha Kifo cha Mtoto Huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe ACP Fulgence Ngonyani Amesema Tukio Hilo Limetokea Agosti 26 Mwaka Huu Majira ya Saa Tano Asubuhi Katika Eneo la Mashujaa Mjini Makambako Baada ya Mbwa Kufukua Mwili wa Mtoto Huyo.

ACP Ngonyani Amesema Mnamo Agosti 23 Mwaka Huu Mtuhumiwa Alijifungua Mtoto wa Kiume na Siku ya Agosti 26 Mwaka Huu Alimfukia Ndani ya Shimo na  Kwamba Upelelezi Dhidi ya Tukio Hilo Linaendelea , Mtuhumiwa Atafikishwa Mahakamani Pindi Upelelezi Huo

Utakapokamilika. 

Katika Tukio Lingine Jeshi Jeshi Hilo Linamshikilia Charles Mbata Kwa Tuhuma za Kuchoma Moto Mali Mablimabli Ikiwemo Shamba la Miti Zaidi ya Hekari 50 Pamoja na Ng'ombe Watatu Zenye Thamani ya Shilingi Milioni 20 na Laki Tano Mali ya Bwana Kaini Nyigu.

Aidha Jeshi Hilo Pia Linawatafuwa Watuhumiwa Wengine Wanaotuhumiwa Kuhusika na Wizi wa Ng'ombe Watano  Wenye Thamani ya Shilingi Milioni Nne Mali ya Inocent Ngole Mkazi wa Mtaa wa Maheve.


No comments: