Afisa mtendaji wa kata ya Nkomang'ombe Bw.Optatus Haule akiwa katika mlango wa chumba cha dawa wa Zahanati ya Nkomang'ombe ambao umefungwa kutokna na ukosefu wa dawa
Huu ni mlango wa chuma cha dawa katika moja ya zahanati wilayani Ludewa kutokana na ukosefu wa dawa
Zahanati ikiwa imefungwa na haina muhudumu kutokana na ukosefu wa dawa
moja ya Zahanati ikiwa imefungwa kutokana na ukosefu wa dwa
Hali imekuwa mbaya katika vituo vya Afya wilayani Ludewa katika
mkoa wa Njombe kwa ukosefu wa Dawa ambapo wananchi wanaoishi vijijini maisha
yao yako hatarini kutokana na MSD kutopeleka dawa katika wilaya hiyo kuanzia
Septemba 2012.
Akizungumza na mwandshi wa gazeti hili afisa mtendaji wa
kata ya Nkomang’ombe Bw.Optatus Haule alisema imefikia wakatati vilango ya
zahanati ya kata hiyo inafungwa kutokana na kutokuwa na dawa hali ambayo
inahatarisha maisha ya wananchi.
Bw.Haule alisema tokea mwezi wa tisa mwaka jana ndipo mgao
wa mwisho ulipafanyika lakini kuanzia hapo zahanati yake haijawahi kupata dawa
na hakuna duka la dawa katika kata hiyo hali inayowalazimu wananchi kwenda mkoa
jirani wa Ruvuma kutafuta dawa.
Alisema hivi karibuni ulitokea mlipuko wa homa za matumbo za
kuhara nakutapika takribani siku mbili hali hiyo iliwalazimu wenye uwezo wa
kununua dripu mkoa jirani wanunue ili dripu moja itumike kwa wagonjwa wawili.
Alizitaja kata jirani zisizo na dawa kama kata yake ni kata
ya Luilo,Masasi na Iwela ambapo wangonjwa kutoka kata hiyo wamekuwa wakitembea
kwa miguu umbali wa zaidi ya kilomita 20 ili kupata msaada wa dawa lakini bado
ni vigumu upatikanaji wa dawa hizo.
“Kwa kweli tumekuwa na wakati mgumu kwa zahanati yetu na
zile za jirani kutokuwa na dawa takribani miezi mitano hivi sasa kwani akina
mama wajawazito na watoto wanapata shida sana na hivi karibuni kutokana na
ukosefu huo wa dawa motto mmoja alifia njiani akipelekwa hospitari ya
wilaya”,alisema Bw.Haule.
Mwananchi mmoja Bi.Ignasia Haule mkazi wa kata ya Iwela
akitoa ushuhuda kutokana na hali hiyo ilivyo mbaya kutokana na ukosefu wa Dawa
alisema alisafiri na motto wake kutoka kata ya Iwela ili aje kupata matibabu
katika Zahanati ya kata ya Nkomang’ombe lakini hali ilikuwa mbaya kama
alikotoka.
Hivyo ikamlazimu kusafiri hadi kata ya Luilo na kuwaomba
msaada Watawa wa kanisa Katoliki Parokia ya Luilo ndipo alipoweza kupata msaada
wa kutibiwa mtoto wake hivyo wananchi wanapata taabu kwa ukosefu huo wa dawa.
Aidha mganga mkuu wa wilaya ya Ludewa Dkt.Happiness Ndosi
akitoa ufafanuzi kutokana na uhaba huo wa dawa katika zahanati alisema MSD ndio
waliochelewa kuzisambaza dawa hizo na lilikuwa ni tatizo ya wilaya nzima.
Dkt.Ndosi alisema Halmashauri ilijitahidi kununua dawa na
kuzisambaza maeneo mengine kutokana na maeneo hayo kuwa na tatizo kubwa hivyo
katika zahanati nyingine haikuwezaka na zikawa zinasubiri mgao wa msd.
Aliwataka wananchi wa kata zisizo na dawa kuvuta subra kwani
tayari msd wameshaanza kusambaza dawa hivyo katika zahanati hizo zisizo na dawa
kabisa zitapewa kipaombele kwa kupata dawa hizo haraka iwezekanavyo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment