Mashindano ya mpira wa miguu ligi daraja la pili yameendelea
kutimua vumbi leo katika viwanja vya wilaya ya Ludewa ambapo timu ya Kurugenzi
Ludewa likuwa ikichuana na timu ya National kutoka kata ya Lugarawa na kutoka
sale ya 2-2.
Akifungua mchezo huo wa mvunguko wa pili katibu wa chama cha
mpira wa miguu Mkoa wa Njombe(NJOREFA) alisema kuwa mpira ni amani upendo maana
michezo hujenga undugu hivyo hatarajii mzunguko wa pili wa ligi hiyo kuwa na
rufaa nyingi.
Bw Njowoka aliwataka waamuzi kuendesha mchezo huo vizuri kwa
lengo la chama cha mpira wa miguu Mkoa ni kuona kila timu inashinda kwa juhudi
zake na si upendeleo kutoka kwa waamuzi kwani ikitokea hali hiyo mwamuzi huyo
atafungiwa michezesha mashindano hayo.
Kutokana na matokeo hayo mwalimu wa timu ya Kurugenzi
Bw.Agrey Mwinuka alisema amelizia maamuzi yaliyotolewa na waamuzi tatizo kubwa
la timu yake kutoka sale katika uwanja wa nyumbani ni kutokuwa na mazoezi ya
pamoja kutokana na wachezaji wake kwenda likizo kwa muda mrefu.
Bw.Mwinuka alisema kuanzia sasa timu yake imeingia kambini
kujiandaa na michezo inayofuata hivyo kwa matokeo hayo anaamini atafanya
mazoezi zaidi ili hali hiyo isijirudie tena katika michezo inayofuata hasa ya
nyumbani.
Aidha kwa upande wa mwalimu wa timu ya National toka Lugarawa
Bw.Comfort Kayombo alifurahia kupata sale hiyo licha ya kuwa timu yake ilikuwa
ikiongoza kwa magoli mawili kwa moja na baadae timu ya Kurugenzi kusawazisha goli
hilo.
Magoli ya timu hizo kwa upande wa timu ya Kurugenzi goli la kwanza lilipatikana kwa penati baada
ya mchezaji wa timu ya National kuunawa mpira karibu na goli lake na goli la
pili lilifungwa kwa mpila wa klosi ambapo mshabuliaji wa timu ya kurugenzi
alilifunga kwa kichwa.
Na kwa upande wa timu ya National mambo yalikuwa vivyo hivyo
ni baada ya mchezaji wa Kurugenzi kumchezea rafu mshambuliaji wa National ndipo
walipo pata penati ya kwanza na kushindwa kufunga goli lakini wakabahatika
kupata penati nyingine kwa kosa hilo hilo ndipo wakapata goli la kwanza na goli
la pili lilitokana na klosi ambapo mchezaji wa National alifunga kwa kichwa.
Mashindano hayo yanaendelea ambapo siku ya kesho timu ya
Luponde fc inatarajia kuvaana na timu ya polisi Ludewa katika viwanja vya
michezo vya wilaya ya Ludewa.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment