Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

January 30, 2013

DIWANI WA CHADEMA AWAFUNDA WANANCHI WA LUDEWA

Diwani mteule wa kata ya Mlangali kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo Bw.Faraja Mlelwa amewataka wananchi wa wilaya ya Ludewa kutoogopa kujiunga na vyama vya upinzani kwa kuhofia vyama hivyo husababisha vita.

Alisema kumekuwa na makada wa chama tawala wanaowatisha wananchi kuwa vyama vingine viko kwaajiri ya kuanzisha vurugu,jambo hilo ni la uzushi kwani bila vyama pinzani maovu ya chama tawala yasingeweza kuonekana hivyo wananchi wanapaswa kuviamini vyama hivyo.

Hayo yamezungumzwa hivi karibuni na Diwani huyo wakati anaapishwa na kufuatia mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya  michezo wilayani hapa.

Bw.Mlelwa aliwataka madiwani wenzake kuacha kasumba ya kushabikia vyama wakati wa baraza la Halmashauri ya wilaya na badale yake kufanya kazi waliyotumwa na wananchi kwani mwisho wa siku wananchi watawauliza kazi walizozifanya na si ushabiki wa vyama.

Aliyasema hayo kufuatia Balaza hilo kuwa na idadi kubwa ya madiwani wanaotoka cham tawala na madiwani wawili pekee wanatoka vyama vya upinzani ambo ni Bw.Kiowi wa kata ya Lupingu akitokea chama cha TLP na Faraja Mlelwa wa kata ya Mlangali akitokea CHADEMA.

"Naomba ieleweke hivi kwa wananchi vyama vyote viko nchini kisheria hivyo iko siku moja nchii hii itatawaliwa na CHADEMA au vyama vingine hivyo asitokee mtu wa kuwatisha pia Madiwani wenzangu tufanye kazi tuliyotumwa na wananchi na si vinginevyo",alisema Bw.Mlelwa.

Bw.Faraja aliwataka madiwani hao kuwa na kaulimbiu ya Ludewa kwanza chama baadae ili kuharakisha maendeleo ya wilaya hiyo iliyoko nyuma kimaendeleo tofauti na wilaya nyingine hapa nchini.

mwisho.

No comments: