Na Nickson Mahundi,Ludewa
Waziri wa nchi ofisi ya Rais mahusiano na Uratibu Mh.Steven
Wassira ameshangazwa na ripoti ya wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe iliyosomwa na mkuu wa
wilaya hiyo Bw.Juma Madaha kuwa zaidi ya wanafunzi elfu mbili hawajui kusoma
wala kuandika.
Taarifa hiyo imesomwa wakati wa ziara ya Waziri Wassira
wilayani Ludewa katika kukagua miradi ya kimaendeleo inayosimamiwa na TASAF
THREE pamoja na MKURABITA ambapo ziara hiyo ilianzia katika shule ya sekondari
Luana na itaendelea kesho.
Katika taarifa yake mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Madaha
alizitaja changamoto wanazokabiliana nazo kwa upande wa elimu ni pamoja kuwa na
wanafunzi zaidi ya elfu mbili wasiojua kusoma na kuandika wakati juhudi za
kulimaliza tatizo hilo zinaendelea.
Hali hiyo ilimfanya Waziri Wassira kushikwa na mshangao
ambapo ilimpasa kumuuliza mtoa taarifa kuwa hao wisiojua kusoma nakuandika
kwanakwendaje katika shule za Sekondari na inakuwaje wahitimu elimu ya msingi
kwa hali hiyo.
Bw.Mdaha alijibu kuwa
kutokana naukosefu wa walimu unaoikumbu wilaya hiyo ndio sababu kubwa
zinazofanya wanafunzi wafikie hatua hiyo lakini uongozi wa wilaya umepanga
mipango ya kulimaliza tatizo hilo.
“tatizo hilo tunalo lakini tumeandaa mpango wa kuwashawishi
vijana wanaohitimu kidati cha nne kwa masharti maalumu kuwapeleka katika vyuo
vya elimu ili wamalizapo masomo yao warudi kufanya kazi katika shule
zetu”,alisema Bw.Madaha.
Adha mradi wa TASAF umetumia zaidi ya shilingi za kitanzania
milioni 42 katika ujenzi wa vymba vya madarasa,jingo la utawala pamoja na
ujenzi wa matundu manne ya choo katika shule ya Luana ambapo ukarabati wa majengo hayo umeshamalizika.
Akitoa hotuba yake Mh.Wassira alisema Serikali imeamua kuungana
na wananchi katika kuleta maendeleo vijijini kwa kutoa fedha lakini
kinachotakiwa wananchi wenyewe wanapaswa kuibua miradi na kuiombea fedha.
Alisema fedha za TASAF hutumika kununulia mahitaji ya
viwandani katika ujenzi lakini wananchi huchangia nguvu kazi ili kupata
mafaniko ya miradi mbalimbali nchini kwani nchi hujengwa na wananchi wenyewe.
Aidha aliwataka vijana wa wilaya hiyo kuunda vikundi
vitakavyowawezeshz kujiajiri katika kilimo cha matunda na mbogamboga ambapo
wataweze kazisafirisha bidhaa zao kutoka wilayani Ludewa hadi kiwanja cha ndege
Songwe Mbeya na kuuza nje ya mkoa.
Ziara hiyo inatarajia kuendelea katika Kijiji vya Shaurimoyo
kata ya Lugarawa na Kijiji cha Amani kata ya Mundindi ambako kunamiradi ya
TASAFU na katika kijiji cha Amani Mh.Wassira anatarajia kukabidhi hati za Ardhi
za Kimila kwa wananchi na kufanya mkutano wa Hadhara na baadae atarudi mkoani
Njombe.
Mwisho
No comments:
Post a Comment