Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

October 27, 2012

TRA WAKAMATA PIKIPIKI NA MAGARI YASIYOLIPIWA KODI KWA MUDA MREFU WILAYANI LUDEWA

Na Nickson Mahundi.

Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wilayani Ludewa wameanza zoezi la kamata kamata kwa vyombo vya moto kwa wamiliki wa vyombo hivyo wasiolipia kodi kwa kipindi kirefu kwa kutokuwa na sababu zisizo za msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Meneja wa TRA wilaya ya Ludewa Bw.Nyot a alisema lengo la zoezi hilo ni kukusanya kodi ya Serikali na si vinginevyo,kwani imekuwa ni kawaidia kwa baadhi ya watanzania bila kukamatwa kodi hailipwi.

Bw.Nyota alisema zoezi hilo ni endelevu kwani walishatangaziwa kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari hivyo wasishangae na hawapaswi kulaumu wao kama wamiliki wa vyombo vya moto kutokana na sheria inayowapasa kuvilipia vyombo hivyo.

Alisema wameanza kukamata Pikipiki,magari na matrekta na mpaka sasa baadhi ya wamiliki wa vyombo hivyo wameanza kuchukua hatua ya kuvilipia imiwemo na fain ya kuchelewa kulipa kodi hizo.

“Kuna watu wanalaumu kwa kufanya zoezi hili,sisi hatuna namna kwani kama kuwatangazia mwisho wa kuzilipa kodi hizo tulishatangaza kinachofanyika kwa sasa ni utekelezaji tu na si vingine vyo sisi tuko kazini na nilazima tutimize majukumu ya Serikali”,alisema Bw.Nyota.

Aidha aliwataka wamiliki wa vyombo hivyo vijijini kulipia kodi hizo kwani kuficha vyombo hivyo haisaidii iko siku vitakamatwa na kutozwa fain kubwa kutokana na kutivilipia kwa muda mrefu.

Mwisho

1 comment:

gowele ludewa said...

jamani kodi ni chanzo cha mapato katika nchi au sehemu yoyote, kama tukitambua hilo basi yatupasa kuitoa kwa wakati ili ifanye kazi kwa wakati kuliko kukaa kulalamikia viongozi wetu kuwa maendeleo hatuyaoni wakati miongoni mwa wanao zorotesha maendeleo ni sisi wenyewe wananchi."AVOID ESCAPING FROM TAX BUILD YOUR COUNTRY" kwani mjenga nchi na mvunja nchi ni mwananci mwenyewe.TAKE CARE!!!!!!!!!!!!!!