Na Nickson Mahundi,Njombe
Shirika la Maendele la taifa(NDC) kupitia mradi wake wa
PAACA limeanza kutoa elimu kwa wananchi wa wilaya ya ludewa namna ya kujikwamua
kiuchumi na kuweza kuuza mahitaji mbalimbali yanayotakiwa na wawekezaji wa
migodi ya Mchuchuma na Liganga.
Akizungumza katika ufunguzi wa mradi huo mwezeshaji wa
kitaifa wa mradi huo Bw.Deosdedis Mtambalike alisema mradi huo utakuwa wakwanza
katika Afrika Mashariki kwani katika Afrika ni nchi ya Afrika ya kusini ndio
iliweza kuwaandaa wananchi wake kupitia mradi huo.
Bw.Mtambalike alisema Mradi wa PAACA unalengo la kuonesha
namna ya kuwashirikisha wananchi wa kawaida kiuchumi ili waweze kuiona miradi
hiyo mikubwa ni mali yao na si vinginevyo kutokana na ajira na kujiajiri
kutakakotokea eneo hilo.
Alisema wilaya ya Ludewa ina fulsa nyingi hivyo wananchi
wanatakiwa kuelimishwa namana ya kuzitumia filsa hizo kwani wasipowezeshwa
watabaki kuwa watazamaji kwa wageni watakonufaika na migodi hiyo.
“NDC imeona ni vema kuwaandaa wananchi wa wilaya ya Ludewa
kwani wawekezaji wanahitaji mahitaji mbalimbali yakiwemo mahitaji ya chakula na
vifaa vya ujenzi hivyo mradi wa PAACA umeanzia Ludewa na utaenea maeneo mengine
ya migodi nchini”,alisema Bw.Mtambalike.
Awali mkurugenzi wa NDC wa Viwanda mama Bw.Aley Mwakibolwa
alisema miradi mingi ya migodi hutoa kodi tu Serikalini hivyo wananchi
wanatakiwa kushiriki kikamilifu katika migopdi ili kujiletea maendeleo kwa
kujiajiri na kuajiriwa.
Bw.Mwakibolwa alisema NDC imejipanga kwa kusambaza elimu ya
kujianda na ujio wa wageni wa migodi ili wananchi waweze kuwa na maisha bora
kwa kuwatoa wataalamu kutoka Ufaransa na maeneo mengine.
Alisema kampuni ya wachina imeainisha mahitaji wanayotaka
kutoka kwa wananchi mahitaji hayo ni Unga,Matunda,Mboga za majani,Vitunguu vya
aina zote,Samaki pamoja na Nyama hasa ya Nguruwe kwa muda wote watakao fanya
kazi katika migodi hiyo.
Bw.Mwakibolwa aliwataka wananchi wa wilaya ya Ludewa
kuchukua hatua kupitia elimu watakayoipata katika mradi wa PAACA kuyaandaa
mahitaji hayo ambayo yatawaptia kipato wananchi hao ambachokitawasaidia
kuondokana na umaskini uliokithiri.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha ambaye alikuwa
mgeni rasmi katika uzinduzi huo alilishukuru shirika la maendeleo la Taifa
(NDC) kwa kuuleta mradi huo wilaya kwake kwa mara ya kwanza Afrika Mashariki
katika kuishirikisha jamii.
Bw.Madaha alisema wananchi wa wilaya yake wako tayari kwani
wanatambua kuwa wanafulsa nyingi lakini walikuwa hawajui kipi cha kuanza nacho
lakini kwa kupitia mradi huo watakuwa na jibu la nini kifanyike.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment