Utata mkubwa umezuka katika msiba wa
marehemu Robert Mlongwa baada ya pande mbili za marehemu kuvutana kuhusu
atakapozikwa marehemu.
Akizungumza na mtandao huu ndugu
mmoja wa marehemu ambaye hakutaka kutaja jina lake ameeleza mwili wa marehemu
ulifika alfajiri ya leo ukitokea Dar es salaam alipokuwa akitibiwa marehemu, na
kufikia nyumbani kwa baba yake marehemu kwa jina Mchungaji Mkuchu.
Baada ya hapo baba huyo wa marehemu
alikataa mwili wa marehemu usisafirishwe Tanangozi ambapo ndipo mama wa marehmu
alipozikwa, ambapo pia kumekwisha andaliwa shughuli za maziko na kuamuru kuwa
mwili huo utazikwa katika makaburi ya mtwivila.
No comments:
Post a Comment