IJUE ASASI YA LUDA
Ludende Development Association ni Asasi ya kiraia
iliyosajiriwa kufanya kazi kiataifa, yenye
namba ya usajiri wa 00NGO/ 1211, yenye makao yake makuu katika Kijiji cha
Ludende Wilayani Ludewa, Mkoani Njombe. Asasi hii ilianzishwa mwaka 2005 ikiwa
na wanachama waanzilishi watano.
Asasi
hii ilianzishwa ikiwa na madhumuni ya msingi kama
yafuatayo:-
Kuhifadhi vyanzo vya maji na mazingira vijijini na kuzuia uharibifu wa Mazingira.
Kuhamasisha wanachama na jamii juu ya umuhimu wa
kuanzisha vyama vya Akiba na Mikopo (SACCOS
Kuongeza uelewa wa kisheria kwa watu masikini na watu
wanaoishi katika mazingira magumu.
Kulinda na kutetea haki za binadamu, Utawala bora, na
kufuatilia wajibu wa Serikali kwa jamii.
Kusaidia wanawake, vijana na watoto yatima kwenye
masuala ya kijamii na kiuchumi.
Kupambana na kudhibiti kilimo na matumizi ya Madawa ya
kulevya.
Kutunza na kutoa misaada mbalimabali kwa watu
wanaoishi na VVU/Ukimwi.
Kulinda, kuhamasisha na kuendeleza mawazo ya watu kama
shughuli za mikono, ngoma na miziki ya asili.
Pamoja
na malengo yote hayo tumejitahidi kutimiza sehemu ya hayo malengo kwa kila
tulipopata fursa ya kufanya hivyo kama
ifuatavyo:-
Tumefanya
miradi ya uhamasishaji wa jamii juu ya uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti
kwenye vyanzo vya maji, kupanda miti kwenye maeneo chakavu/nyika na ufugaji
nyuki tangu mwaka 2008 hadi hivi leo, Lakini mwaka 2009 shirika la Umoja wa
mataifa UNDP walitufadhili mradi wa kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa
wanajamii wa kata tatu Ludende, Mundindi na Milo katika wilaya ya Ludewa, kuwatika miche ya miti Laki mbili na kutengeneza
mizinga ipatayo 32; Mradi huu ulifanikiwa sana kwani tulifanikiwa kugawa miche
takribani laki moja na elfu themanini kwa wanajamii wa Tarafa ya Mlangali,
Liganga na Mawengi na Miche nyingine tuliwagawia wanachama wa Asasi ili
kufanikisha zoezi zima upandaji miti na hivyo kuepusha ukame na kulinda
mazingira. Kwahiyo katika sehemu hii ya uhifadhi wa mazingira kwa uhakika
tumefanya vizuri kiasi cha kufikia nusu ya malengo ya miaka mitano
tuliyojiwekea.
Asasi yetu pia imekuwa inafanya miradi ya utoaji elimu kwa jamii juu ya mada
mbalimbali kama vile sera, utetezi na uhamasishaji, katika hili kwanza tulianza
kufanya miradi ya Kisera hasa ile ya utoaji wa Elimu ya Haki
ya mwanamke kumiliki Mali na Ardhi kwa ufadhili wa shirika la The
Foundation For civil society (FCS) mwaka 2009; Hivyo kwa kuwa tulifanikiwa
kufanya kazi nzuri na mfadhili huyu aliendelea kutufadhili kwa kila mradi ambao
tuliomba kufanya hasa kwenye eneo hili la utoaji wa elimu kwa jamii pamoja na
uhamasishaji juu ya haki ya mwanamke kumiliki Ardhi. Kwa mara ya mwisho tulipata mradi mkubwa
ambao bado unatekelezwa wa “Haki ya
mwanamke kumiliki ardhi” ambao kimsingi utachukua miezi tisa kumalizika
(utaisha Desemba 2012).
Hata
hivyo tunakusudia kufanya vizuri kwa kila lengo tulilojiwekea ingawa kwa sasa
tunaenda hatua kwa hatua na kuchukua lengo moja baada ya jingine ili kuifikia jamii nzima ya Ludewa na
kupunguza kero za wananchi ambazo ni vikwazo kwa maisha yao ya kila siku.
Huu
mradi tuufanyao tunatarajia kufanya kwa mkoa mzima lakini kwa awamu kutegemeana
na uwezo wa wafadhili kwa kila hatua kwani tamaduni zetu zinawatenga wanawake
katika kumiliki mali na hasa mali ya ukweli ambayo ni Ardhi, na lengo letu ni
kuondoa mfumo dume huo na kuleta usawa katika jamii nzima hasa katika umiliki
wa ardhi, kwani pia tunatambua msemo
usemao kuwa kumwelimisha mwanamke ni
kuelimisha jamii nzima, na kwa mantiki hiyo kumkomboa mwanamke ni kuikomboa
jamii nzima.
Mwisho
No comments:
Post a Comment