MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI JAJI WEREMA AJIUZULU
Wiki chache zilizopita wakati Kikao cha
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kikiendelea, macho ya watu
wengi na masikio yalikuwa na hamu ya kutaka kuujua mwisho wa sakata la
Escrow.
Wakati watu wengi wakisubiri maamuzi
yatakayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya
Kikwete kuhusiana na Ripoti juu ya issue ya ubadhilifu wa fedha kwenye
akaunti ya Escrow, leo December 16 kuna taarifa iliyotufikia muda mfupi
iliopita kuhusu kiongozi mmoja wa Serikali kujiuzulu.
Taarifa iliyoripotiwa na kituo cha ITV inasema
aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
amejiuzulu siku ya leo na barua yake tayari imefika Ikulu ambapo Rais
Kikwete ameridhia maamuzi hayo na kumshukuru kwa uamuzi huo kwa kuwa
ushauri wake kuhusiana na suala la Tegeta Escrow haukueleweka.
No comments:
Post a Comment