Mwenyekiti mpya wa CCM kata ya Milo Bw.Joel Mhagama.
Vijana
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wamepania kukibadirisha chama cha
mapinduzi kwa kuchukua uongozi katika nafasi mbalimbali ndani ya kata na vijiji
ili kuendana na kasi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyekiti
wa CCM Taifa Dkt.John Pombe Magufuli.
Hayo
yamedhihirika leo baada ya mmoja wa vijana hao Bw.Joel Mhagama ambaye ameibuka
kidedea katika uchaguzi wa nafasi ya Mwenyekiti wa ccm kata ya Milo wilayani
hapa kwa kuwabwaga washindani wake katika nafasi hiyo ambapo washindani hao
walionekana kuwa na umri mkubwa tofauti na kijana huyo.
Akiongea na
mwandishi wa mtandao huu mara baada ya kuibuka mshindi Bw.Joel Mhagama alisema
kuwa ni mkakati ambao vijana waliuandaa ili kuchukua nafasi mbalimbali za kata
na vijiji ndani ya chama ili kuendana na kasi ya kimaendeleo ya mwenyekiti wa
chama wa Taifa.
Bw.Mhagama
alisema kuwa wilaya ya Ludewa imekuwa na viongozi wazuri wa chama kwa muda
mrefu lakini wengi wao walikuwa ni wazee kutokana na ukweli kwamba vijana
wamekuwa wakiogopa kugombea nafasi hizo na kuwaacha wazee wakizikalia kwa mika
yote lakini kutokana na hali halisi ya kasi ya kiutendaji ya sasa nafasi hizo
zinapaswa zishikwe na wanaoweza kuendana na kazi ya Mwenyekiti wa Chama wa
Taifa.
Alisema kuwa ameibuka mshindi kwa kupata kura 44 wakati aliyemfuata amepata kura 22 na wa mwisho alipata kura 3,kwa ushindi huo umempatia ujasiri wa kuona kumbe wajumbe wamemuamini kuwa anaweza hivyo kazi aliyonayo ni kuwarudisha vijana ambao walikwenda vyama vya upinzani ili waweze kuijenga kata ya milo kwa kauli moja.
“nimewasinda
wenzangu kwa kura nyingi niwaombe washindani wangu ushirikiano mkubwa kutoka
kwao ili kata yetu ya Milo isonge mbele kimaendeleo awali niliogopa sana
kugombea nafasi hii lakini nikajipatia ujasiri ambao umenifikisha hapa,nawaomba
vijana wenzangu walishinda chaguzi za vijiji na kata kuwatumikia wananchi bila
ya kujali itikadi za vyama vya siasa”,alisema Bw.Mhagama.
Aidha
Bw.Mhagama ambaye ndiye mwenyekiti mpya wa ccm kata ya Milo aliwashukuru
wajumbe aliomchagua na ameupongeza mfumo unaotumika ndani ya chama kwa sasa wa
kukomesha Rushwa na viashiria vyake ili kuwapata viongozi kwa haki.
mwisho
No comments:
Post a Comment