Bw.Yohana Nkwera akionesha miguu yake iliyo hivi sasa
Haya ndio Makazi ya Bw.Yohana Nkwera na Dada yake
Hii ndiyo baiskeri yake anayoitumia hivi sasa
Bw.Yohana Nkwera akiwa na miguu yake ya bandia pembeni
Bw.Yohana jinsi anavyoweza kuitumia miguu yake ya bandia
Mwandishi wa habari wa kituo cha radio cha Best fm Ludewa Bw.Albentino Kayombo pamoja na Bw.Crement Lugongo ambaye ni jirani wa Yohana wakimsaitia kuiweka vizuri miguu hiyo ya bandia ambayo tayari imechakaa
Bw.Crement Lugongo(Msela) jirani wa Yohana Nkwera.
Mkazi mmoja
wilayani Ludewa katika kijiji cha Ludewa k mkoani Njombe Bw.Yohana Nkwera(54)anaomba
msaada kwa wadau mbalimbali wanaoweza kumsaidia kujengewa Nyumba ya Kuishi na
Baiskeli ya walemavu wa miguu kutokana na maswahibu yaliyomkuta anayoyataja ni
mambo ya kishirikina baada ya kukatika miguu yake miwili akiwa usingizini na
kutotoka damu.
Akiongea na
mwandishi wa habari hii Bw.Yohana alisema kuwa ni miaka zaidi ya ishirini sasa
amekuwa akipata mateso makali baada ya miguu yake kukatika bila ya kutokwa na
damu kwani chanzo cha kukatika miguu hiyo ni mgogoro baina yake na mzee mmoja
ambaye jina lake limehifadhiwa ambapo mgogolo huo ulipelekea mzee huyo kutoa
maneno mazito ya kumtoa viungo vya mwili.
Alisema kuwa
siku moja akiwa amelala alihisi maumivu makali ya miguu lakini alipoamka
asubuhi aliona iko kawaida lakini inauvimbe mdogo tu,alikwenda Hospitari ya
wilaya ya Ludewa na kuonana na madaktari na baada ya kupimwa walimueleza kuwa
hakuwa na tatizo,lakini usiku wakuamkia siku pili alisikia maumivu tena ndipo
ilipofika asubuhi nyingine aliikuta miguu yake ikiwa imekatika maeneo ya
magotini na ikiwa pembeni.
Aliongeza
kuwa hali hiyo iliishangaza jamii ya Ludewa kijijini lakini ndugu na jamaa
walichangishana fedha na kumsafirisha kwenda hospitari ya Ikonda iliyoko wilaya
ya Makete lakini mambo bado yalikuwa magumu ikalazimika apewe Baiskeli ya
walemavu wa miguu na kurudi kuanza maisha mapya ya kutofanyakazi na kubaki
nyumbani huku akisaidiwa na dada yake ambaye mpaka sasa ndiye anayemsaidia
richa ya kuwa dada yake huyo ni mzee sana.
“Naomba
msaada kwa watu wenye mapenzi mema kwani nilipewa miguu ya bandia nayo tayari
imechakaa,nyumba ninayoishi msimu wa mvua inavuja sana pia baiskeri
yakutembelea tairi wajanja wameniibia na kutoa vifaa vingine hata kula kwangu
ni shida hivyo naombeni msaada wenu kwani hali yangu ni mbaya mno”,alisema
Bw.Yohana.
Aidha Jirani
yange Bw.Crement Lugongo(Msela) alisema kuwa bw.Yohana walisoma wote akiwa na
afya Njema na hakuwa na ulemavu wowote kwani walianza darasa la kwanza mwaka
1971 na alikuwa mchezaji mzuri wa mpira
wa miguu na mpigaji wa ngoma ya bendi lakini ilishangaza sana baada ya miaka
kadhaa kukatika miguu bila hata ya kuugua na haikutoka damu.
Bw.Lugongo
alikiri kuwepo kwa imani za kishirikina kwani ni ni jambo la ajabu lililomkuta
bw.Yohana hivyo amekuwa akiishi maisha magumu kwani hata godoro la kulalia ni
tatizo hivyo majirani humsaidia chakula na luezeka nyumba yake kwa nyasi pale
nyasi zinapochakaa na kuhitaji kubadirishwa.
Alisema kuwa
msaada mkubwa ulenge katika ujenzi wa nyumba yakuishi kwani hata Dada yake umri
umemtupa mkono hivyo kama wadau watajitokeza kumsaidia hata kumjengea kibanda
kidogo ambacho kitaezekwa bati basi anaweza kuwa na maisha mazuri kwani
hajawahi kuoa mpaka sasa katika maisha yake.
Namba ya
kumchangia ni 0752206242 Nickson Mahundi na 0659615635 Albentino Kayombo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment