TCRA YADAI MITANDAO INAYOWEKA HABARI ZA UONGO, NA PICHA CHAFU INAWEZEKANA KUIFUNGIA
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), Profesa John Nkoma alipokuwa akifungua warsha ya siku moja kwa
wafanyakazi wa mamlaka hiyo katika kuadhimisha Siku ya Mteja inayofikia
kilele chake leo.
Alisema matumizi mabaya ya mawasiliano ndiyo yanayofanywa kuwapo kwa
taarifa za uzushi na uchochezi, picha na video zisizo na maadili.
“Tatizo hapa si huduma za simu, intaneti, instagram au whatsapp,
tatizo ni utumiaji usiofaa unaofanywa na baadhi ya watu. Tunahitaji
elimu ya kutosha kwa jamii ya namna ya kutumia vizuri huduma hizi,”
alisema.
Alipoulizwa kwa nini Tanzania isiifunge mitandao kama ilivyo China na
baadhi ya nchi za kiarabu, Nkoma alisema jambo hilo linawezekana lakini
linahitaji fedha nyingi na litarudisha nyuma maendeleo.
Naye Mkurugenzi wa Masuala ya Watumiaji na watoa huduma, Dk Raynold
Mfungahema akitoa mada ya majukumu ya TCRA, alisema pamoja na kukua kwa
sekta ya mawasiliano, bado huduma zinazotolewa haziridhishi hivyo
kuhitaji uwekezaji zaidi.
Aidha, alisema mamlaka yake imekuwa ikipokea malalamiko kadhaa kutoka
kwa wateja wa mawasiliano na kubwa ni kuibiwa fedha kwenye simu,
kubadilishiwa namba, ujumbe usiohitajika, kutopatikana kwa namba ya
huduma kwa wateja, matumizi ya ving’amuzi na madhara ya minara na simu.
No comments:
Post a Comment