Makamba: Enzi za ushindi wa kishindo CCM zimepita
Siku chache baada ya matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuonyesha kuwa CCM, imeporomoka, Mbunge wa Bumbuli, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba amewataka wanachama wa chama hicho kujiandaa kisaikolojia kwa matokeo yoyote yanayoweza kutokea katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.
“Wana-CCM wanatakiwa kujiandaa
kisaikolojia kwani walizoea ushindi wa asilimia 90 au 80 (wa kishindo),
huu ulikuwa ushindi wa nyuma. Tusishangae tukipata ushindi wa asilimia
50, 60, 57 au 70 ni kitu cha kawaida kutokana na kukua kwa demokrasia
hususan ushindani wa vyama vingi vya siasa kuanza kuimarika:-Makamba
Kauli hiyo ya Makamba imekuja wakati matokeo ya serikali za mitaa
yakionyesha kuwa CCM imeporomoka kutoka ushindi wa asilimia 91.7 mwaka
2009 hadi 79.8 katika uchaguzi wa mwaka jana na upinzani ukipanda kutoka
asilimia nane mwaka 2009 hadi takriban 20 mwaka jana.
Akizungumza jana katika mahojiano na kipindi cha ‘Power Breakfast’
cha Redio ya Clouds na baadaye kufafanua alisema matokeo ya uchaguzi huo
ni ishara kwamba kwa umri wa miaka 22 sasa, mfumo wa vyama vingi vya
siasa umeanza kuimarika.
“Hata
ushindi wa asilimia 81 tulioupata katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa
bado ni mkubwa na hata kama tungepata asilimia 70 haupunguzi uhalali wa
uongozi. Kusema CCM itang’oka madarakani, hapana, bado wananchi
wanakiamini tena sana:-Makamba.
Chanzo Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment