baadhi ya wananchi waliofika nyumbani kwa marehem
Askari wa
jeshi la Polisi kituo cha Ludewa mjini ambaye alikuwa lindo la bank ya NMB
mwenye namba G.6352D/C aliyefahamika kwa
jina moja la Abduel anasadikika kumuua
kwa kumpiga risasi na bunduki aina ya SMG kijana mmoja aliyefahamika kwa
jina la January Mtitu (20) usiku wa kuamkia tarehe 23/01/2015 nyumbani kwa
kijana huyo.
Tukio hilo
limetokea baada ya Askari huyo kutoroka lindo na kwenda nyumbani kwa marehemu maeneo
ya Ludewa mjini mtaa wa Mdonga usiku wa saa sita na kufanya uharifu huo hali
ambayo imewashtua wananchi wa mji wa Ludewa ambao hawajawahi kuona matukio kama
hayo yakifanyika katika mji wao.
Hali hiyo
imesababisha baadhi ya wananchi kutaka kufanya maandamano ya amani kupinga
kitendo hicho cha kulaani jeshi la polisi kumuua mwananchi asiye na hatia na
pia wamesusia kuchonga sanduku la kuuzika mwili wa marehemu huyo wakitaka jeshi
la polisi wilayani Ludewa lihusike katika mazishi ya mwananchi huyo.
Akiongea kwa
masikitiko mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye ni dada wa marehemu January
aliyejitambulisha kwa jina la Imani Mtitu alisema marehemu alisikika akibishana
na watu katika simu yake ya mkononi kwa muda mrefu majira ya saa sita usiku na
baada ya mabishano hayo watu hao walimweleza tunakuja huko kwako naye akasikika akiwajibu njooni.
Imani
alisema Baada ya dakika chache walisikika watu akigonga mlango wa chumba cha
kaka yake na kuamua kuuvunja ndipo mabishano yakaendelea huku marehemu
akisikika kuwa anasema anaadhibiwa kwa kosa asilolijua ndipo ikasikika sauti ya
risasi na marehemu akilalamika kwa uchungu.
Baada ya kukamilisha
tukio hilo alisikia vishindo vya watu vikikimbia ndipo alipoamua kufungua
mlango wake bila mafanikio kwani ulikuwa umefungwa kwa nje na wauaji hao
akaamua kutumia njia ya kutoka dirishani na kwenda katika chumba cha kaka yake
ambapo alimkuta akiwa amelala chini na ametapakaa damu,alijaribu kumuuluza ni
akina nani waliofanyia tukio hilo hakuweza kujibu kutokana na hali mbaya
aliyomkuta nayo ndipo alipoamua kuwaita majirani na kuanza kuwafuatilia wauaji
hao ambao walionekana wakikimbia ikiwa moja amevaa sale za jeshi la polisi na
mwingine akiwa na mavazi ya kiraia.
“nilisikia wakiongea
tunakuua tupo tayari kufukuzwa kazi mara iukasikika mlio wa bunduki katika
chumba cha marehemu kaka yangu nilipojaribu kufungua mlango wangu ulikuwa
umefungwa kwa nje nakaamua kupitia dirishani na kwenda haraka katika chumba cha
kaka na kumuona akiwa tayari hajitambui nikawaita majirani kuwafuatilia wauaji
tulifanyikwa kuwaona watu wawili mmoja amevaa nguo za polisi na mwingine nguo
za kawaida wakikimbia”,alisema Imani.
Alipo ulizwa
mkuu wa wilaya ya Ludewa ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama
Bw.Juma Solomon Madaha alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwataka wananchi
kutuliza jazba kwani bado uchunguzi kamili wa chanzo cha tukio hilo unaendelea
na baada ya kukamilika wananchi watataarifiwa kuwa nini kinaendelea.
Alisema wananchi wanatakiwa kuwa wapole kwani jeshi la polisi na vyombo vingine vya kiusalama vinaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha tukio hilo.
Alisema wananchi wanatakiwa kuwa wapole kwani jeshi la polisi na vyombo vingine vya kiusalama vinaendelea na uchunguzi ili kujua chanzo cha tukio hilo.
Endelea
kufuatilia mtandao huu kujua nini kinaendelea wilayani Ludewa.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment