Imeelezwa
kuwa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ipo hatarini kuanguka katika uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika Octoba 2015 kutokana na kuwanyanyasa waalimu kwa
kutowapa stahiki zao ikiwa ni pamoja na madai ya fedha za
likizo,nauli,kupandishwa madaraja na nyongeza za mishahara.
Kauli
hiyo imetolewa jana na mwenyekiti wa chama cha waalimu wilayani
Rungwe,Elizabeth Sikila alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
Serikali kuwatelekeza kwa kutowapa stahiki zao mbali na kuwa amefikisha suala
hilo kwa viongozi husika.
Sikila
ambaye pia ni mwalimu wa shule ya msingi Madaraka iliyopo wilayani humo,alisema
waalimu wanahali ngumu na wengi wao wamekata tamaa ya maisha kutokana na
kufanya kazi katika mazingira magumu huku Serikali ikishindwa kutambua majukumu
waliyo nayo.
Aliyataja
madai hayo kuwa ni,Milion 26 za likizo na nauli kwa waalimu wa shule za
sekondari ambapo walilipwa Milion 4 tu,na kuwa Milioni 46 za waalimu wa shule
za msingi ambazo walikuwa wakizidai toka mwezi juni mwaka 2013 ambapo walilipwa
milioni 20.1 tu kwa awamu mbili.
Mwenyekiti
huyo alidai kuwa fedha hizo wanazodai zimetokana na nauli zalikizo,kuhamishwa
vituo vya kazi na fedha za madai mbalimbali pamoja na nyongeza za
mishahara na kwamba waalimu walioongeza viwango vya elimu bado hawajapandishwa
madaraja.
Aliongeza
kuwa katika ziara ya katibu mkuu ccm Taifa Abrahamani Kinana alipozuru wilayani
humo alitoa lalamiko hilo pamoja na kumkabidhi daftari la madai lakini bado
madai hayo hayajapatiwa ufumbuzi hali inayowakatisha tamaa ya kujituma katika
majukumu yao ya kikazi.
Alisema
kwa hali hiyo Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inajiweka katika mazingira ya kupata
anguko kubwa katika uchaguzi mkuu na kwamba waalimu ndiyo chachu ya ushindi
katika chaguzi zote na kama hawajamalizana na waalimu wasitegemee ushindi.
‘’Mimi
ni mwanachama wa ccm lakini kwa mtindo huu sipo tayari kuendelea kukisapoti kwa
kuwa mambo yote yafanywayo na Serikali yanatekeleza Sera ya chama hicho, hatupo
tayari kuendelea kukisapoti chama hicho wakati Serikali yake inatutesa kwa
kutotupa stahiki zetu,alisema mwenyekiti huyo.
Alisema
wilaya ya Rungwe ina jumla ya shule 244 kati ya hizo shule za msingi ni 51 na
vyuo viwili vya ualimu na kuwa katika vyuo hivyo Serikali imevitelekeza kabisa
wakufunzi wanaishi maisha ya tabu baada ya serikali kutozitatua kero zao.
Aliongeza
kuwa walipeleka kero zao kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya pamoja na mkurugenzi
lakini bado hawajapatiwa tiba ya namna ya kuondolewa kero zao kutokana na
serikali kutokuwa sikivu na wanaipeleka nchi pabaya kwa kuwatenga waalimu.
‘’haiwezekani
watu wachache waharibu mabilioni ya nchi kwa kufanya ufisadi alafu wananshindwa
kuwaadabisha na kuzirudisha fedha hizo ambazo zingeondoa kero za waalimu na
kuongeza miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Mkurugeza
mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Veronika Kessy mbali na kukiri kuwepo
kwa madai hayo ya waalimu alisema kuwa suala hilo ni janga la Taifa na kuwa
walikwisha yapeleka madai yao kwenye wizara husika na yanafanyiwa kazi.
No comments:
Post a Comment