Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

December 18, 2013

MABANDA YA WAFANYABIASHARA NYUMA YA STENDI YA MJI WA NJOMBE YAMEANZA KUBOMOLEWA




 Zoezi la Ubomoaji wa Mabanda Ukiendelea


  Serikali Mjini Njombe Imeanza Kutekeleza Zoezi la Ubomoaji wa Mabanda ya Wafanyabiashara wa Vyakula na Nguo Aina ya Mitumba Yaliyopo Nyuma ya Kituo cha Mabasi Mjini Njombe Katika Kuuweka Mji wa Njombe Katika Hali ya Usafi na Usalama Zaidi.

Hatua Hiyo Imekuja Kufuatia Kituo Hiki Kufuatilia Kwa Ukaribu na Utekelezaji wa Zoezi Hilo Lililo Takiwa Kutekelezwa Tangu Mwezi Novemba Mwaka Huu Jambo Ambalo Lilishindwa Kufanyika.

Akizungumza na
mtandao huu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Edwin Mwanzinga Amesema Kuanza Kutekelezwa Kwa Zoezi Hilo Iwe ni Muendelezo wa Kuhakikisha Eneo Hilo Linakuwa Safi na Hivyo Ameutaka Uongozi wa Mtaa wa Gwivaha Mjini Njombe Pamoja na Mambo Mengine Bwana Mwanzinga Amesema Kuwa Eneo Hilo Kwa Akali Kubwa Lilikuwa Likitumika Kwa Mambo Ya Uhalifu Ikiwemo Kutumika Katika Utumiaji wa Madawa ya Kulevya,Ulevi na Kutumia Kama Vyoo.

Kwa Upande Wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Gwivaha  Mjini Njombe Bwana Nathanael Maxona Amesema Kuwa Ifikapo Disemba 19 Mwaka Huu Siku ya Alhamisi Zoezi Hilo Litakuwa Limekamilika Kwa Kuyaondoa na Kuyapanga Mabanda Hayo Kulinga na Biashara Wanazo Zifanya.


  Na Gabriel Kilamlya Njombe

No comments: