KAMPUNI ya Tanzania
China International Minerals Resouces Limited iliyoundwa na ubia kati ya
Tanzania na china inashindwa kuanza machimbo ya makaa ya mawe ya mchuchuma na
chuma cha Liganga kutokana na serikali kushindwa kutimiza masharti yaliyomo
ndani ya mkataba imefahamika.
HUANG DAXIONG afisa
mtendaji wa kampuni alizungumza hayo jana katika kambi ya machimbo ya makaa ya
mawe Mchuchuma alisema kazi waliyoitarajia kuifanya inaendelea lakini
wanakumbana na changamoto ambazo mtatuzi ni Serikali ya Jamuhuri ya Tanzania.
Bw.Daxiong aliyataja
makubaliano ya kampuni yake na Serikali ni pamoja na upanuzi wa barabara kuu
kutoka Njombe hadi Nkomang’ombe ambako ndiko kwenye makaa ya mawe.
Alisema wanashindwa
kupitisha mitambo ya kufanyia kazi kutokana na barabara hiyo kuwa nyembamba na
madaraja mdogo ambapo ni vigumu kupitisha gari zenye tani kubwa katika barabara
ya wilaya ya Ludewa.
“makubaliano yetu na
Serikali ilikuwa ni upanuzi wa barabara haraka iwezekanavyo ili tuweze kufanya
kazi ambayo inategemea zaidi kusafirisha mitambo kutoka bandari ya Dar es
salaam hadi migodini lakini sisi tumeshaanza kazi Serikali ya Tanzania
bado”,alisema Daxiong.
Aidha alizitaja
changamoto nyingine ni pamoja na urasimu ulioko bandari ya Dar es Salaam katika
kuchukua mitambo yao inayotoka nchini China na ucheleweshaji wa vibari vya
kufanyia kazi.
Bw.Daxiong alisema
urasimu huo ulioko Bandarini pamoja na ucheleweshaji wa vibari umekuwa
changamoto kubwa kwao kwani mitambo mingi bado iko bandarini na haijulikani
hatma ya tatizo hilo kwani muda unazidi kwenda bila mafanikio.
Alisema suala la
vibari lilianza kushughurikiwa kabla ya kusaini mkataba lakini kumekuwa na
urasimu mkubwa ambao unawakatisha tama wawekezaji hao katika kuifanya kazi hiyo
ya uanzishaji wa mgodi kwa wakati muafaka kama walivyotarajia.
Bw.Daxiong alimuomba
mbunge wa jimbo la Ludewa Bw.Deo Filikunjombe kujaribu kuishawishi Serikali ili
kuharakisha vibari vya kazi,upanuzi wa barabara na kuondoa urasimu bandarini
ili waweze kuondoa mizingo yao haraka pindi inapofika bandarini hapo.
Nae Filikunjombe
aliahidi kuongea na Serikali ili kuharakisha miradi hiyo ambayo ni miradi
mikumbwa nchini kwani umeme utakozalishwa mchuchuma utatumika nchi nzima na
ndio suruhisho la tatizo la umeme nchini.
Filikunjombe aliitaka
kampuni hiyo kutokatishwa tama na mambo hayo kwani Serikali inayoongozwa na
rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete iko makini ila kuna watu wachache ndio tatizo
ambao hawana maisha marefu ndani ya Serikali hiyo.
Bw.Filikunjombe
aliwataka wananchi waishio katika maeneo ya migodi kuwapa ushirikiano
wawekezaji ili waweze kuiona Tanzania ni nchi yenye maziwa na asali na wananchi
wake ni wakalimu kama tamaduni za mtanzania zilivyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment