Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw.Deo Filikunjombe alimweka
kitimoto kaimu muhandisi wa maji wilaya Bw.Theodory Mfuse mbele ya wananchi wa
kijiji cha maholong’wa na kumtaka atamke ni sababu zipi zilizopelekea wananchi
wa kijiji hicho licha ya kutoa michango yao mpaka sasa hawana maji safi na
salama hali ainayopelekea wananchi hao kuto iamini Serikali yao.
Bw.Filikunjombe alifanya hivyo kutokana na kijiji hicho
kilichopo kata ya Ludende kutokuwa na maji kwa muda mrefu licha ya kuwa na
fedha za miradi ya maji ambazo zilitengwa kusambaza miundombinu ya maji katika
kata hiyo yenye vijiji vitatu lakini fedha hizo zimetumika katika kijiji cha
Ludende pekee na kushindwa kufika katika vijiji vingine.
Alisema Serikali haita fumbia macho ubadhilifu unaoonekana
wazi wazi kwani ofisi ya maji wilaya ya Ludewa imeshindwa kuwafishia wananchi
wa kijiji cha Madindo na Maholong’wa maji safi na salama kutokana na uzembe
kwani hata mchoro wa ramani kuonesha wapi miundombinu ya maji itapita limekua
tatizo hilo ni tatizo kubwa ndani ya ofisi hiyo.
Bw.Filikunjombe alimuelea Mfuse kuwa wananchi hao wako tayari
kutoa nguvu zao katika uchimbaji wa mitaro ya kupitisha mabomba na tayari wana
zaidi ya shilingi milioni tatu(3) bank ambazo walichangishana kwaajili ya
upatikanaji wa majisafi na salama lakini mamlaka ya maji wilaya ya Ludewa ndio
tatizo kubwa katika kuchelewesha utekelezaji.
“mimi nashangaa ni miaka mingi sasa imepita hakuna
kinachoendelea mmeweka mabomba mpaka kijiji cha Madindo lakini hakuna maji pia
wananchi wa Maholong’wa waliwaomba muwacholee ramani ili watafute mfadhiri kama
ninyi mmeshindwa lakini mpaka sasa hakuna hiyo ramani,nataka uwaeleze wananchi
katika mkutano huu ni lini mtakamilisha kazi hiyo”,alisema Bw.Filikunjombe.
Alisema mradi huo wa kusambaza maji katika vijiji vitatu vya
kata ya Ludende ulikuwa mkubwa na fedha za mradi wa maji zilitoka Bank ya Dunia
lakini kuna baadhi ya watu ndani ya sekta hiyo wamefanya ndivyo sivyo hivyo
Serikali haitaweza wafumbia macho watu wa namna hiyo kutokana na wananchi
wanavyoiamini Serikali yao.
Aidha kaimu mwandisi huyo alipata wakati mgumu mbele ya
wananchi katika kulijibia hilo kutokana nay eye ndiye aliyekuwa msimamizi wa
ujenzi wa mradi huo uliotakiwa kupeleka maji katika vijiji vitatu na badara
yake maji yalifika kijiji kimoja na kijiji kilichofuata kutandikwa bomba zisizo
na maji.
Bw.Mfuse alijitetea kwa kusema fedha za ujenzi wa mradi huo
zilikuwa zikija kwa awamu hivyo awamu ya kwanza ilikuwa ni ujenzi wa tank ambao
ulikamilika,awamu ya pili ilikuwa ni kusambaza miundombinu ya kupitishia maji
katika vijiji viwili yaani kijiji cha Ludende na Madindo na awamu ya tatu
ilikuwa ni kijiji cha maholongwa lakini fedha hizo hazikuletwa.
Alikili kuwepo na uzembe katika uandaaji wa ramani ambayo
iliombwa na uongozi wa kijiji hicho ili kupeleka kwa mfadhiri ambaye aliahidi
angeweza kulitatua tatizo la maji katika kijiji hicho hivyo atalifanyia kazi
haraka iwezekanavyo ili wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali yao.
Nae Diwani wa kata ya Ludende Bw.Frank Luoga Mseya alisema ni
miaka mitatu imepita ofisi hiyo ya maji imeshindwa kutekeleza ombi la kijiji
hicho la uchoraji wa ramani hali hiyo inaonesha ofisi hiyo inaurasimu kwani
kila viongozi wa kijiji wakifika ofisini hapo kufuatilia ramani hupata ahadi
zisizotimilika.
“wananchi wanaona kama Serikali inawatenga kwani kjiji
kikubwa kama hiki tokea nchi ipate uhuru haijawahi kupata maji safi na salama
zaidi ya kuugua homa za matumbo na wengine kupoteza maisha kutokana na kutumia
maji yasio salama”,alisema Bw.Frank Luoga Mseya.
Bw.Filikunjombe alisisitiza kuwa kama yeye ni mbunge wa jimbo
la Ludewa aliiomba ofisi hiyo impe makisio ya usambazaji maji katika mji wa
Ludewa mpaka sasa ni miezi sita imepita
hajapata makisio hayo ni dhahiri wasingeweza kuwapa ramani wananchi wa kijiji
cha Maholong’wa.
Hivyo alimtaka kamimu muhandisi huyo kuhakikisha wananchi wa
kata hiyo wanahudumuwa ipasavyo na si ahadi kwani wanafedha zao walizochangishana
zitakazo wasaidia katika utatuzi wa kero hiyo kwani wako tayari kujitolea nguvu
zao katika kufanikisha suala la maji.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment