WATUMISHI katika
hospitali ya misioni ya Lugarawa
wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wanalazimika kufanyakazi bila kupumzika
kutokana na uhaba na upungufu mkubwa wa wafanyakazi wa kada mbalimbali hususani
watabibu na wataalam wengine.
Akizungimza na gazeti
hili jana mganga mkuu wa hospitali hiyo inayomilikiwa na kanisa katoliki jimbo
la njombe Dr Daudi Mwakalago alisema hospitsli yake inakabiliwa na changamoto
nyingi ikiwemo waganga ambapo hadi sasa anao waganga wasaidizi(Asissitant
medical officers) wawili na mganga msaidizi (medical assistant ) mmoja tu.
‘’’’kutokana na uhaba
huo waganga tunalazimika kufanyakazi masaa ishirini na nne bila kupumzika
lakini kwa upande wa wauguzi hali siyo mbaya sana ukilinganisha na maafisa
uuguzi hivyo tunaomba kuongezewa wathumishi ili kuongeza tija.’’’ Alisema
Mwakalago
Aidha mwakalago
akaongeza kuwa mbali na uhaba wa wauguzi katika hospitali hiyo bado wanakabiliwa
na changamoto nyingine ya ugumu wa uendeshaji hospitali kwa sababu wananchi wengi wa eneo hilo
wanakabiliwa na umaskini wa kipato hali inayowafanya washindwe kumudu gharama
za matibabu na kupelekea wengine kutoroka bila kulipia huduma za matibabu na kusababisha hasara.
Kwa kawaida Hospitari yetu hupokea wagonjwa mbalimbali
wanaokuja kupata huduma hata kama hawana fedha lakini kwa makubaliano ya kulipa baadaye
lakini hukosa uaminifu na kuamua kutoroka bila kulipa ‘’’’’watu wetu kipato
chao ni duni kwa hiyo siyo wote
wanaolipa madeni wengi wanatoroka kwa kushindwa kulipia gharama za
matibabu.’’’alilalamika Mwakalago
Alizitaja gharama za
matibabu kuwa mama mjamzito anayejifungua kwa upasuaji (operation) ni shilingi elfu
thelathini na tano(35,000)akina mama wanaojifungua kawaida shilingi elfu kumi
na tano (15,000), upasuaji kwa wagonjwa wa kawaida ni shilingi sabini
elfu(70,000) zikiwemo gharama za malazi.
Kwa wagonjwa ambao ni
wanachama wa bima ya afya wanalazimika kulipa shilingi laki moja na sitini
elfu(160,000) kiwanga ambacho ni kidogo sana ukilinganisha na sehemu zingine za
mjini.
Dkt.Mwakalago alisema
Hospitali hiyo iliyoanzishwa na wamisionari bado inakabiliwa na changamoto
nyingi ikiwemo upungufu wa wafanyakazi na kukosa fedha za kujiendesha kutokana
na kukosa ufadhiri kwa muda mrefu sasa.
Kuhusu fedha toka Serikalini alisema Hospitari hiyo
haijapata fedha hizo zaidi ya miezi saba
sasa hivyo uendeshaji wa kazi katika vitengo vya mama na mtoto umekuwa mgumu
ambapo inawalazimu kuwatoza kiasi cha shilingi elfu tano kwa watoto katika
kuchangia huduma za Afya.
Licha ya changamoto
zinazo ikabili Hospitali hiyo Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw.Deo Filikunjombe
ametoa msaada wa mashuka 162 ambayo yatatumiwa katika vitanda vya wagonjwa
wanaolazwa katika hospitali hiyo.
Akitoa msaada huo
Bw.Filikunjombe alisema ameguswa na changamoto zinazoikabili hospitali hiyo
hivyo ameona vi vema kuona uwezekano wa kupunguza changamoto hizo na akaahidi
ataendelea kufanya linalowezekana ili kuendeleza historia ya Hospitali ya
Lugarawa.
Bw.Filikunjombe
alijumuika na wagonjwa katika chakula cha mchana ili kuwafariji katika sikukuu
ya X mas kwani aliweza kuona kazi wanazofanya wafanyakazi wa hospitari hiyo
bila ya mapumziko kutokana na uchache wao.
Akishukuru kwa msaada
wa mashuka na kandambili pea 100 alizozitoa Bw.Filikunjombe Dkt.Mwakalago
alisema ni upendo wa kipekee aliouonesha Bw.Filikunjombe wa kutoa msaada huo na
kula chakula na wagonjwa hivyo jamii inapaswa kuiga tabia hiyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment