WAKULIMA na wananchi
wilayani Ludewa katika mkoa mpya wa Njombe wametakiwa kujiandaa kwa kujinunulia
mbegu, mbolea ya kupandia na kukuzia badala ya kutegemea ruzuku na pembejeo
kutoka serikalini kwa haiwasaidii chochote.
Akizungumza katika
baraza kuu la madiwani lililofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa halmashauri
ya wilaya hiyo, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Matei Kongo
aliwataka wakulima kuondoa mawazo ya kutegemea mbolea ya ruzuku kwani serikali imezidisha
mizengwe badala ya uwajibikaji.
MATEI KONGO, mbegu,
mbolea ya kupandia na kukuzia imekuwa ikiwafikia wakulima mwezi machi wakati
mvua zinamalizika, badala ya kuwafiki oktoba mvua zinapoanza kunyesha. hii
haina tija kwa mkulima na hakuna sababu ya kuendelea kuimba wimbo wa kilimo
kwanza kwani ni udanganyifu mkubwa.
Kongo akaongeza kuwa
pamoja na ruzuku ya pembejeo kutomfikia mkulima kwa wakati, wananchi wamekuwa
wakikumbana na udanganyifu ikiwemo uchakachuaji na wizi vitu ambavyo
vinaendelea kuididimiza mkulima na kuwanufaisha watu wachache wakiwemo mawakala
na maafisa watendaji wa vijiji na kata.
Akitoa ufafanuzi
kuhusu pembejeo kwa msimu huu mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha akawaambia
madiwani hao kuwa utaratibu wa utoaji pembejeo kwa msimu huu umebailika ambapo
mawakala hawatatumika tena badala yake makampuni makubwa ndiyo yatakayo husika
kusambaza pembejeo.
Aurelian Mhagama ni
mkulima wilayani Ludewa, kwa upande akaitaka serikali kupata mawazo ya wananchi
ambao ndiyo wahitaji wa pembejeo badala ya kuwapangia wakulima wakiwa maofisini
jambo linaloleta mkanganyiko mkubwa kwa sababu wakulima wanatekeleza mipango
ambayo wao hawakushiriki kuibua na kuipanga.
Hadi sasa mvua
zimeshaanza kunyesha lakini hakuna dalili yoyote ya ruzuku ya pembejeo toka serikalini,
hakuna sababu ya kuendelea kusubiri huruma ya serikali kwa sababu hali
inaonesha kuwa ruzuku siyo haki ya wakulima.
Nao madiwani wakapaza
sauti na kuilalamikia serikali kuwa hakuna sababu ya kuendelea kuwadanganya
wakulima wakati hawaoni faida ya ruzuku badala yake wanashuhudia watu wachache
wakinufaika na wanapopelekwa mahakamani hushinda kesi na kuendelea na wizi huo.
Wilaya ya Ludewa
imegawanyika katika tarafa tano na kata ishirini na tano ambapo inategemea sana
mazao ya chakula huku zao kuu likiwa
mahindi.
mwisho
No comments:
Post a Comment