A: SUALA LA KAMATI YA LIGI
CHAMA
cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimeamua kulipeleka
kwa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT), suala la
kuzuia televisheni na redio kutangaza moja kwa moja michezo ya Ligi Kuu
Tanzania Bara pamoja na wapiga picha za televisheni kuchukua picha kwa
ajili ya kutumia kwenye habari.
Hatua
hiyo ya TASWA ina lengo la kuomba mwongozo kwa
chama hicho ambacho ndio kinachomiliki vyombo vya habari kuhusiana na
suala hili ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa kiasi kikubwa na wanachama
wetu.
Tayari
TASWA imefanya mazungumzo ya awali na MOAT, ambayo imeridhia iandikiwe
barua rasmi ili jambo hilo lijadiliwe kwenye vikao vyake na baada ya
hapo TASWA itapewa mwongozo ambao itautoa kwa waandishi wa habari za
michezo.
Kwa
kuwa Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto pia ni mjumbe wa MOAT, basi suala
hilo tunaamini litafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo, hivyo tunawaomba
waandishi wa habari za michezo waendelee kuwa watulivu na wavumilivu
kipindi hiki na wafanye majukumu yao kama kawaida.
Siku
zote chama chetu kimekuwa na uhusiano mzuri na Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF) na wadau wengine wote na TASWA haitaki ifike mahali iwe
na mgogoro na chama chochote cha michezo, lakini pia haitakuwa tayari
kuona wanachama wake wakishindwa kutekeleza majukumu yao.
Kama
mnavyojua wiki iliyopita kulifanyika kikao cha Kamati ya Ligi na baadhi
ya klabu zinazoshiriki ligi hiyo kuhusiana na tukio la kuzuia
televisheni na redio kutangaza moja kwa moja michezo ya Ligi Kuu pamoja
na wapiga picha za televisheni kuchukua picha kwa ajili ya kutumia
kwenye habari.
Katika
kikao hicho ambacho Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto alihudhuria
kulitoka maelezo mbalimbali ambayo baadhi ya wanahabari hawakubaliani
nayo na wamekuwa wakitaka
TASWA ichukue hatua uamuzi mgumu.
Sekreterieti
ya TASWA imeona si vizuri kukurupuka kuchukua uamuzi wowote ule kwa
sasa kwani yenyewe haina chombo cha habari, lakini wanaofanya kazi
kwenye vyombo vya habari ndiyo wanachama wake. Itawasilisha MOAT
maazimio ya kikao cha Kamati ya Ligi kuhusiana na jambo hili, tuna
hakika tutalimaliza.
B.MKUTANO MKUU
Jumatano
Novemba 16, 2012 Kamati ya Utendaji ya TASWA itakutana Dar es Salaam
kupitia
ajenda za Mkutano Mkuu wa chama chetu, kisha Jumatatu Novemba 18
Mwenyekiti wa TASWA atafanya mkutano na wanahabari kutangaza mdhamini wa
mkutano huo pamoja na tarehe rasmi na mahali utakapofanyika.
Kutokana
na kuandaliwa kwa ajenda mpya ya kuboresha chama na maslahi ya
wanachama wake, TASWA inaendelea kutafuta wadhamini zaidi ili kuufanya
mkutano huo uwe wa siku mbili.
Nawasilisha.
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
No comments:
Post a Comment