Ikiwa ni siku kadhaa zimepita tokea uanzishwe mradi wa PACA
inaotekelezwa na shirika la maendeleo la Taifa (NDC)tathmini ya mradi huo wa
ushirikishwaji wa wananchi katika maendeleo ya wilaya yao imeonyesha kufanya
vizuri tofauti na hapo awali.
Akizungumza katika kikao cha tathmini hiyo mwezeshaji wa
kitaifa wa maradi huo Bw.Deosdedis Mtambalike alisema kama kila
mwanaludewa atajitambua kuwa anapaswa
kuhusika katika ujenzi wa uchumi wa wilaya yake basi mradi huo utakuwa mkombozi
wa mwananchi wa hali ya chini.
Bw.Mtambalike alisema kuwa maradi huo ni wakwanza
kutekelezwa katika Afrika mashariki ukiwa na lengo la kuwashirikisha wananchi
katika ukuaji wa uchumi ndani ya maeneo
yao ili kuondoa migogoro kati ya wawekezaji na wananchi walioko katika maeneo
ya migodi.
Alisema kumekuwa na mogogoro mingi katika migodi hapa nchini
na Afrika kwa ujumla kutokana na kutowafanyia maandalizi yakutosha wananchi
kujiona wao ni sehemu ya migodi hiyo kutokana na hilo Tanzania ameamua kuandaa
wananchi wake katika kukabiliana na hilo.
“mpango huu wa Serikali kama utafanyiwa kazi kama
ilivyokusudiwa basi wananchi wa wilaya ya Ludewa watakuwa mfano kwa wilaya
nyingine zenye migodi ya madini kwani wilaya hii ina fulsa nyingi ambazo
zikifanyiwa kazi wananchi wake watajitoa katika umaskini haraka”,alisema
Bw.Mtambalike.
Mradi huo unalengo la kuwahusisha wananchi katika uzalishaji
wa mahitaji mbalimbali yanayohitajika kwa wafanyakazi wa migodini ikiwemo
ufugaji,kilimo na usindikaji ambapo wananchi wataweza kijipatia fedha kupitia
uuzaji wa bidhaa migodini.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Ludewa Bw.Juma Madaha alisema hatma
ya uchumi wa wilaya ya Ludewa uko mikononi mwa wananchi wa wilaya ya ludewa kwa
kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa mradi huo kupitia shirika la NDC.
Bw.Madaha alisema yeyote aliyepata mafunzo ya mradi wa PACA
naye ataitwa PACA kwa kuisambaza elimu hiyo kwa wananchi wengine alioko
vijijini ili kila mmoja aweze kujihusisha kwa namna moja au nyingine katika
uzalishaji ndani ya wilaya yake.
Hata hivyo kampuni ya Wachina inayojihisisha na uchimbaji wa
migodi ya makaa ya makaa yam awe yaliyoko mchuchuma na chuma cha liganga ilitoa
mahitaji ya wafanyakazi wake ikiwa ni unga,nyama,matunda,mboga za majani
,samaki na nyama.
Mahitaji hayo yamekuwa ni adimu kuwafanya wafanyakazi hao
kuagiza mbali na wilaya ya Ludewa ili kufanikisha kuwa na chakula cha kutosha
kwa wafanyakazi wa migodi hiyo hali ndio inayochochea wananchi kupewa elimu ya
ujasiliamali na uzalishaji kupitia mradi wa PACA ili waweze kunufaika na miradi
hiyo.
Bw.Mtambalike aliwataka wafanya biashara kujenga hotel za
kisasa na kujenga viwanda vya usindikaji wa vyakula kwani bila kufanya hivyo
watabaki kuwa watazamaji katika migodi hiyo amabyo ni mikubwa na itakayofanya
kazi hizo kwa miaka mingi.
mwisho
No comments:
Post a Comment