UPATIKANAJI
wa huduma za Afya hasa huduma ya mama na mtoto katika Zahanati ya kata ya
Luana wilayani Ludewa limekuwa ni tatizo kubwa ambapo huwalazimu kutembea zaidi
ya kilomita 10 kuifuata huduma hiyo Ludewa Mjini.
Hayo
yalisemwa na Afisa mtendaji wa kijiji cha Luana Bw.Ladislaus Morani katika
kikao kilichoandaliwa na shirika la Daraja kuhusiana na mpango wa shirika hilo
katika kufanya tafiti ya huduma za afya zitolewazo vijijini.
Bw.Morani alisema
wananchi wa kata Luana hasa akina mama wamekuwa wakipata shida katika huduma ya
chanjo hivyo huwalazimu kutembea umbali mrefu kufuata huduma hiyo.
Alisema
akina mama wazawazito wamekuwa wakisafirishwa na usafiri wa pikipiki (bodaboda)na
wakati mwingine hujifungulia njiani hali hiyo ni hatari kwa akina mama hao
kwani wanaweza kupoteza maisha yao au ya mtoto kutokana na Hospitari ya wilaya
kutokuwa na gari ya wagonjwa inayoweza kutoa msaada wa haraka kwa wagonjwa
.
Bw.Morani alisema
zahanati hiyo ambayo inamilikiwa na kanisa katoliki haina dawa kwa muda mrefu
sasa hivyo kwa mgonjwa yeyote katika kata hiyo hutakiwa kununua dawa katika
duka moja tu lililopo katika kata ya Luana.
“wananchi wa
kijiji chetu hasa akina mama wamekuwa na shida ya huduma ya chanjo ya wao
wanapokuwa wajawazito na watoto wao hali inayowalazimu kusafiri hadi Ludewa
mjini kufuata huduma hiyo,lakini hata dawa na usafiri hatuna na tukiwasiliana
na hospitali ya wilaya tunaelezwa hakina gari”,alisema Bw.Morani.
Akizungumza
katika kikao kilichowakutanisha wadau wa Afya katika zahanati nne wilayani
Ludewa kaimu Mkurugenzi wa shirika Daraja lenye makao yake makuu mkoani Njombe Bw.Simon
Mkina alisema shirika lake linafanya kazi ya kutoa msukumo kwa Viongozi na
watendaji wa Serikali kutoa huduma stahiki katika jamii.
Bw.Mkina
alisema mpango wao ni kukutana na wadau katika zahanati kumi na sita ndani ya
mikoa miwili ikiwa ni kufanya utafiti
katika sekta ya Afya ili kubaini mambo mazuri na mapungufu ikiwa ni
mojawapo ya kazi za shirika hilo katika kuhamasisha utendaji bora ndani ya
Serikali.
Alisema
kumekuwa na changamoto kubwa katika sekta ya afya hivyo tafiti inayofanya na
shirika la Daraja inaweza kuibua mambo mengi hasa zahanati na vituo vya afya
vilivyoko vijijini kutokana na maeneo mengi kusahaulika katika huduma hizo.
“tumeanza
kufanya tafiti katika mikoa miwili ya kuanzia lakini matokeo yatakayopatikana
katika mikoa hii tunaamini ni ya nchi nzima na baada ya hapo tutatoa taarifa
katika Halmashauri husika ili wajirizishe na taarifa yetu na baada ya hapo
taarifa hizo zitatolewa katika vyombo mbalimbali vya habari ili kuujulisha uma
nini tunakifanya”,alisema Bw.Mkina.
Bw.Mkina
alisema kupitia ufadhiri wa watu wa Marekani mpango huo utafanikiwa ikiwa kila
mwananchi na mdau wa Afya ataeleza ukweli kuhusiana na huduma zitolewazo ambapo
watahitaji kujua upatikanaji wa dawa,wafanyakazi wa sekta ya afya kama
wanakidhi mahitaji,upatikanaji wa maji safi katika dhahanati,vyombo vya usafiri
kwa wagonjwa na mapungufu katika nyumba za wafanyakazi na motisha zao.
Akifungua
kikao hicho Mganga mkuu wa wilaya Ludewa Dakt.Hapines Ndossi alisema wilaya yake inakabiliwa na changamoto nyingi
ambazo utafiti huo utabaini,lakini changamoto kubwa anayokabiliana nayo ni
upungufu wa wafanyakazi ambapo wamekuwa wakiacha kazi kutokana na mazingira ya
kazi kuwa magumu.
Dr.Ndossi
alisema wilaya ya Ludewa inazaidi ya vituo vya Afya 50 ambavyo vinachangamoto
ya upungufu wa watumishi na nyumba za kuishi watumishi hali ambayo inawakatisha
tama wananchi waliojitolea nguvu zao kuvijenga vituo hivyo.
Alisema
Halmashauri ya wilaya inampango wa kutekeleza sera ya Serikali ambayo imelenga
kujenga zahanati kwa kila kijiji ili kupunguza vifo vya akina mama wajawazito
vinavyotokana na kusafiri umbali mferu kaajili ya kutafuta huduma ya Afya.
Aidha
aliwataka viongozi wa shirika la Daraja kabla ya kuitendea kazi ripoti ya
utafiti wanaoufanya ni vyema wakaipeleka kwa uongozi wa wilaya ndipo isambazwe
maeneo mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment