Social Icons

Facebook Twitter LinkedIn Google+

October 29, 2012

MLEZI WA CHADEMA MKOA WA IRINGA NA NJOMBE BW.THOMAS NYIMBOAJIENGUA


Bw.THOMAS NYIMBO AKIONGEA NA WANANCHI MKOANI NJOMBE


Mlezi  wa  chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) mkoa  wa Iringa na Njombe Thomas Nyimbo amejiengua rasmi Chama hicho kwa madai  kuwa  kimeshindwa  kumuenzi Daud Mwangos aliyeuawa katika tawi alilolifungua yeye tawi la Nyololo wilayani Mufindi..

Nyimbo ameeleza kuwa siasa ya kumwaga damu  za watanzania   kama  kifo cha Mwangosi  yeye  aliguswa  sana na hata  kumpigia simu mbunge wa jimbo la Iringa mjini Peter Msigwa na kumtaka  kusimamia msiba  huo lakini hakufanya  hivyo na badala yake alinyamaza  kimya hata ujumbe  alioutaka  kumfikishia katibu mkuu wa Chadema Dr Slaa hakufikisha ndio sababu ya  kuchukia na kuamua kukaa kando .


Hivyo  amesema kuwa kutokana na mauaji hayo yaliyosababishwa na Chadema wenyewe yeye kama mlezi  wa Chadema mkoa  wa Iringa na Njombe ameamua  kutojihusisha na chadema na kukaa kama mwanasiasa  huru asiyefungamana na chama chochote cha  siasa .


Hata  hivyo amesema   siasa ya Tazanzia kwa  sasa ni lazima  watanzania kuchagua mtu na sio Chadema ama CC M wala chama chochote cha siasa ili kuondoa vurugu za kisiasa zinazoendelea kwa  hapa nchini.


"katika bango langu la kugombea ubunge mwaka 2010  niliandika mtu kwanza chama baadae na niliandika chagua Nyimbo wala  sikusema chagua chama ila eneo dogo sana niliweka chagua Chadema ila lengo ni  watu kuchagua mtu sio  Chadema"


Nyimbo alisema alisema kuwa hata M4C ya  Chadema haina malengo kwa ajili ya mtanzinia bali ipo kwa ajili ya Chadema  wenyewe  hivyo kama kweli Chadema  wanataka hiyo harakati yao ni vema ikawa ya  watanzania sio ya kifamilia ama ya  watu binafsi .


Asema  kuwa hii M4C ya Chadema itamaliza  watanzania iwapo hawatakuwa makini kwani haipo kwa ajili ya kuleta amani ya  watanzania  na kudai  kati ya miaka 10 mwanachama mpya aliyejiunga na Chadema ni yeye Thomas Nyimbo pekee  hivyo lazima watanzania  kujiuliza kwanini Chadema haipati wanachama  wapya .


Hivyo alisema  kuwa nchi inaangmizwa na ufisadi wa baadhi ya  viongozi na ndio sababu ya vijana  kukimbilia Chadema ila  iwapo ambo yatawekwa  sawa  Chadema sio  Chama katika Tanzania.

No comments: